NIDA kusitisha matumizi ya namba kwa wasiofuata vitambulisho vyao

Kama upo nje ya mkoa ulioandikisha utaratibu ukoje ?
 
Wale wazee ambao hawajaenda kuchukua Vitambulisho ambayo viko tayari vyao ni muda wa kwenda kuvifata maana Nida wametoa taarifa kwenye ukurasa wao wa Instagram watazifungia namba:

====================================================

KUCHUKUA KITAMBULISHO CHA TAIFA KATIKA OFISI YA NIDA YA WILAYA YAKO
Itakumbukwa kuwa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) iliendesha zoezi la uzalishaji mkubwa na usambazaji vitambulisho vya Taifa kwa umma kuanzia Oktoba 12, 2023 hadi Machi 2024 kwa kuvipeleka vitambulisho hivyo katika ofisi za watendaji wa Kata, Vijiji, Mitaa Vitongoji na Shehia na kuwataka wananchi kujitokeza kwenda kuvichukua katika ofisi hizo chini kote.

Hata hivyo pamoja na NIDA kupeleka vitambulisho hivyo katika Kata, Vijiji, Mitaa, Vitongoji na Shehia ili kuwarahishishia wananchi kuchukua vitambulisho vyao, bado kuna wananchi hawajajitokeza kuvichukua hali iliyosababisha vitambulisho vyao kuendelea kubaki katika ofisi hizo kwa muda mrefu sasa.

Kwa kuzingatia hilo, Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa inawatangazia wale wote ambao hawajajitokeza kuchukua vitambulisho vyao na watakaopokea ujumbe mupi wa maandishi katika simu zao (sms), kufika katika ofisi za NIDA za wilaya walikojisajili kuchukua vitambulisho vyao kama itakavyoelezwa katika ujumbe huo.

Atakayeshindwa kufanya hivyo matumizi ya Namba ya Utambulisho wake wa Taifa (NIN) yatasitishwa baada ya mwezi mmoja tangu kupokea ujumbe huo.​
 

Ule ubabaishaji wetu kazini kwa mara nyingine tena.

Kwani namba ina kazi gani kumbe?

Dawa ya moto ni moto, Wacha wasitishe tuone nani ataula ugali bila mboga!
 
Hivi inawezekana mtu akaenda kukuchukulia?
Wanachukuliana bila pingamizi.

Changamoto mchukuaji akikipoteza na kutomfikishia mhusika ndipo ilipo shida yenyewe.

Hakuna despach book inayotumika kuchukuliana ili kukiri ushahidi wa kimaandishi.
 
Wanachukuliana bila pingamizi.

Changamoto mchukuaji akikipoteza na kutomfikishia mhusika ndipo ilipo shida yenyewe.

Hakuna despach book inayotumika kuchukuliana ili kukiri ushahidi wa kimaandishi.
Je hakuna sehemu yeyote itakayo hitaji mhusika mwenye kitambulisho kutia saini yake?
 
Bashungwa hana historia ya kukurupuka. Ila kwa hili atakua amejikurupusha kufanya hiyo decision bila kuweka mpango sawa.
How comes mtu atoke mkoa mmoja adi mwingine kufuata tu ID? Imagine gharama ya kutoka DSM hadi Mwanza-Ilemela-Mecco kufuata ID ya almost mwaka 2016/17 kwa
 
Je hakuna sehemu yeyote itakayo hitaji mhusika mwenye kitambulisho kutia saini yake?
Nilivyoona utaratibu ulivyo: kunakuwa na counter boook iliyoorodheshwa vitambulisho vyote vilivyopo, halafu kuna sehemu ya kusaini mchukuaji.

Sasa mtu akifika pale anachambua vya watu anaowafahamu, mf: mke, mtoto, rafiki nk nk, kisha anasaini mbele ya kitambulisho anakichochukua, haulizwi kitambulisho ama utambulisho wake, ni just a sign, anabeba.

Vingine vimechakalia kwenye ofisi za watendaji kwa sababu ya kushikwa shikwa kila siku kwenye kuchambua.
 
Ahaa sawasawa shukran mkuu.
 
Sasa mtu anaenda kuchukua kitambulisho wanamuomba rushwa unategemea nini?
Kwani yeye anafanya hivyo kwa kutumia Sheria gani?
Huyu waziri ni mzigo
 
Mnoanaa Tuna Lazimishana Kurogana sasa sindio Ninyi NIDA ?!..Yaani Nitoke TANGA hadi Dar kisa ID wakati nili Hangaika two months kukitafuta mlipo sema vipo kwenye Serikali za mitaa na sija kipata ?!..Mnakuaga Na Upuuz na Niwapuuzi vile vile.
 
Ivi wakuu kama ID yangu ya NIDA ime expire napatàje mpya?
 
Sema kinafutika kirahisi kweli, uitunze kama mtoto, usipoangalia utajikuta uko na plastiki tupu.
 
Wamefanya vyema wasipochukua wadeactivate NIDA zao kwenyhe system.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…