The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Hili la kutaka kufungia namba za utambulisho wazee mnazingua, wananchi hawajagoma kuchukua vitambulisho vyao.
***
Mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIDA leo imetangaza kuwa itasitisha matumizi ya namba za utambulisho za wananchi ambao hawatachukua vitambulisho vyao baada ya kutumiwa ujumbe mfupi ndani ya siku 30.
Soma pia: NIDA kusitisha matumizi ya namba kwa wasiofuata vitambulisho vyao
Taarifa hii inakuja mara baada ya mamlaka hiyo kuzalisha vitambulisho hivyo na kuvisambaza katika maeneo ambako wananchi walijiandikisha ambapo muitikio wa wananchi kwenda kuchukua umekua hafifu sana.
Mamlaka inatangaza kusitisha matumizi ya namba hizo kwa watu watakaokaidi kwa muda uliotolewa, kwani tatizo ni wananchi kwamba wamegoma kuvichukua? Au mamlaka yenyewe imekosa ubunifu wa njia sahihi ya kuwafikia wananchi walipo?
Mfano mzuri pengine mtu alijiandikisha akiwa Bukoba mwaka 2019, katika harakati za utafutaji anapata mishemishe mkoa mwingine mfano Njombe, leo kitambulisho cha NIDA kimetoka kinapelekwa Bukoba, Je mtu huyu atakubali kwenda Bukoba kwa kutumia gharama kubwa kufuata kitambulisho tu na kuacha kibarua chake kiyeyuke au kazi kusimama? Pitieni hata maoni ya wananchi katika kurasa zenu hili linalalamikiwa.
Kuvifungia matumizi namba hizo si suluhisho kwamba wananchi wataenda kuvifuata, asilimia kubwa ya ambao hawajachukua ni wale ambao wapo mbali na maeneo yao waliyojiandikishia.
Ninawashauri NIDA wasiachwe nyuma na teknolojia, wawasiliane na watu ambao hawajachukua vitambulisho ili kujua maeneo walipo, ili ofisi zilizo karibu yao zitumike kutoa vitambulisho hivyo. Inaweza kuwa kwa kutumia ujumbe mfupi au kupiga simu au katika mfumo wa tovuti ya mamlaka iwekwe sehemu ambayo itamruhusu mtu kuchagua kitambulisho chake akakichukulie wapi tofauti na alipojiandikishia.
Igeni kutoka kwa benki mbalimbali, kadi inaweza ikamezwa Singida ATM ukiwa safarini lakini kesho yake ukiwapigia customer care watakuuliza upo wapi kadi yako iletwe karibu na tawi lao ulilopo hata kama ni Songea huko.