Syston
JF-Expert Member
- Nov 6, 2017
- 243
- 351
Leo uzi wangu naikosoa NIDA hasa katika kipengere hiki cha kuprint ID copy online. Ni jambo zuri na mnastahii kupongezwa kwa hilo ila mtu aliyepitia adha za huduma hii hawezi kuwapongeza, mimi nikiwemo.
Tuanze hivi, nilienda statinary kuprint ID nikaambiwa 4000, nikaona siwezi kuvumilia ujinga wa wafanya biashara wa kibongo kupandisha bei inapotoea dili, basi nikarudi zangu maskani nikaingia NIDA id verfication portal nikadowload ID yangu ili nikai print nipeleke inapohitajika.
Mama weeeee! ikaja katika mfumo wa .gif. Tuzungumzie GIF kidogo, hii ni kifupisho cha GRAPHICS INTERCHANGE FORMAT, ambayo huwa haipotezi ubora wa picha (lossless format), mfano wake ni vile vipicha unaona kitacheza na hakina sauti. Ok huu ni mfumo mzuri wa kuhifadhi ubora lakini hata mifumo mingine kama PNG, JPEG nk nayo haipotezi ubora kiasi cha macho kuona ubora umepungua.
Shida ni kuwa hizi .gif files huwezi kuzifungua moja kwa moja kwenye computer mpaka uwe na software tool, au unajua kucheza na computer (jambo ambalo kwa watanzania lipo kushoto). Hapa nachojiuliza ni kuwa kwa nini NIDA waweke kwenye mfumo huu wakati lengo lao ni kumrahisishia mwananchi mnyonge apate Copy ya ID yake kwa ajili ya matumizi mbalimbali.
Binafsi nimekerwa sana na watu wa stationary maana wamekuwa kama wauza nyama buchani na NIDA ndiyo sikukuu yao. NIDA nadhani mmeliona hili hakuna point ya kuwa na hii service kama mtu hawezi kujihudumia mwenyewe. Sometimes unaambiwa tuma picha ya ID sasa wew mwenyewe huwezi ifungua utamtumiaje mtu ambaye pengine ni ajira au unataka mkopo.
YANGU NI HAYO.