Mwanzoni walihitaji kitambulisho cha kura, baadaye wakahitaji cheti cha kuzaliwa. Na kwasasa wanahitaji tuwe na:
Cheti cha kuzaliwa
Cheti kutoka Migration
Cheti cha kidato cha nne
Cheti cha darasa la saba.
Uwe navyo vyote. Ni halali kweli hii?
======
JamiiForums, imezungumza na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Geofrey Tengeneza kufahamu iwapo wameongeza nyaraka za kukabidhi ili kupata Kitambulisho cha Taifa (NIDA) ambaye ameeleza kuwa taarifa hiyo haina ukweli na siyo sahihi.
"Hiyo siyo kweli na siyo sahihi kabisa, vitu va msingi kabisa kwa jaili ya kusajili kupata kitambulisho cha NIDA ni:-
Hivo vitu vingine ni vitu tu vya kuongeza kama utakuwa navyo mwenyewe kutia nguvu maombi yako na si kwamba kama utakuwa hauna hiyo vya kuongezea hautasajiliwa hiyo si kweli, hata kama huna hivyo vya kuongezea utasajiliwa tu". Geofrey Tengeneza Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)
Pia soma:Vitu 3 muhimu vya kuwa navyo unapoomba Kitambulisho cha Taifa (NIDA)

- Cheti cha kuzaliwa cha mtu anayeomba analeta nakala
- Cheti cha kuzaliwa(nakala) cha mzazi mmojawapo, baba au mama, na kama hawana hicho cheti cha kuzaliwa kama wana kitambulisho cha NIDA cha mzazi mmjowapo baba au mama basi unaambatanisha nakala ya cheti cha NIDA cha mzazi mmojawapo baba au mama. Na kama hawana vyote hivyo cheti cha kuzaliwa au nakala ya NIDA basi unakwenda kwa mwanasheria au mahakamani, anakupa kiapo unaapa kwa jina kinaitwa affidavit kwa ajili ya mzazi mmoja wapo, unaapa kisha unaambatanisha hiyo affidavit.
- Kitu cha tatu cha msingi ni barua ya Serikali za mtaaa unakoishi, kwa hiyo lazima uwe na barua ya Serikali za mtaa unakoishi wanaeleza kwamba wanakutambua kama mkazi katika huo mtaa katika lile eneo.