KERO NIDA Mtwara ni shida, huduma zao zinakwaza, kila siku wanawazungusha watu bila sababu za msingi

KERO NIDA Mtwara ni shida, huduma zao zinakwaza, kila siku wanawazungusha watu bila sababu za msingi

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Ofisi ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Mtwara imekuwa kikwazo sana kwa wateja, hakuna huduma nzuri na mambo meni hayaendi kwa wakati, wanachelewesha mambo hata katika mambo ambayo hayana vikwazo hivyo.

Kuna Mtumishi mmoja anaitwa Neema, huyu amekuwa akiwanyanyasa Watu sana na kuwarudisha kila siku kwa makosa madogo ambayo mhusika anaweza kuyarekebisha muda huohuo.

Anawaambia watu “rudi kesho” wakati amesharekebisha makosa, huyu mtumishi ni jeuri sana, tunaomba NIDA makao makuu, Watu wanalalamika sana.
 
Kwa ufupi ni kwamba "nida mtwara wanatengeneza mazingira ya rushwa" full stop
 
Tunataka watanganyika wa kweli. Na si watu wakutoka msumbiji sawa.
 
Back
Top Bottom