A
Anonymous
Guest
Ofisi za NIDA katika wilaya ya Nachingwea zina matatizo na usumbufu mwingi sana, kuna watu wamepeleka form toka mwaka jana mwezi wa nane lakini cha kushangaza mpaka leo hawajapata namba zao na ukifuatilia wanakuambia kuwa mtandao unasumbua.
Kuna wengine wanaambiwa kuwa watoe elfu 50 kupata namba zao siku hiyohiyo sasa unajiuliza hizo namba zinatoka wapi na mtandao unasumbua?
Wengine wanapeleka form leo wanaambiwa wapeleke wiki inayofuata ukiuliza kwanini leo azijapokelewa hawakupi majibu.
Naomba mamlaka husika itatue tatizo hili maana NIDA ni kitu muhimu kwa mazingira ya sasa.