NIDA nafasi za Kazi kwa Vijana na Volunteers kuondoa Foleni ya Registration

NIDA nafasi za Kazi kwa Vijana na Volunteers kuondoa Foleni ya Registration

Inanambo

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2011
Posts
4,039
Reaction score
2,840
NIDA pamoja na NIA yenu nzuri ya kuwapatia WaTZ vitambulisho naona hili zoezi la uandikishaji linawakera watu kwa kuwa wanapanga foleni ndefu tena juani kila siku wakikimbizana na deadline. zile fomu hazina ugumu wa Kivile wa kutoweza kujazwa na ofisa anayejua kuandika vizuri na siyo mwandiko wa kuku hata kama hakupata semina yenu. Ili kuondoa foleni na malalamiko wapeni Watendaji wa mtaa ruhusa ya kurecruit watu wenye uwezo wa kuandika vizuri kwa hizi siku zilizobaki. Ni bora hata mkatafuta shule ya Msingi au sekondari penye nafasi na meza ili muweze kumaliza zoezi hili kwa ufanisi.Mkijidai kazi mnaweza ninyi tu mtawafanya watu wengi wasijisajili. Kila ofisi ya serikali za mitaa ni foleni ndefu na malalamiko kibao. Mkija mara mnakuja na ofisa mmoja au wawili ambao hawakidhi haja. Toeni nafasi kama N B S walivyofanya kama mna nia kweli ya kuwapa WaTz Vitambulisho.
 
Inategemea na eneo huku mbez beach makonde kuna vijana walopewa tenda wanalipwa ten thou per day.
 
bongo hatuta fika kila kitu siasa! apo watasema umetumwa na chadema
 
ushauri mzr, wajipange vyema, wanachangamoto nyingi zinazo wakabili.
 
Ili mtumie ID zenu za JF
Tatizo hili linasababishwa na wananchi kwa asilimia kubwa, siku za mwanzoni walijitokeza wachache! Nakumbuka hata zoezi la usajili wa line za simu ilikua hivi, inabidi tubadilike.
 
kwa hilo Nida walikuwa na mahesabu mabaya, next time yapasa wajipange kama fursa zingine zitatokea kuhusiana na jamii.Nachelea kusema kwamba hii ni kwa mkoa wa dsm tu. je mikoa hiyo iliyo baki jee???????????????wachukue hatua mapema.
 
Sensa bado itatoa bias data!Matokeo yke ndo wrong plans frm wrong data
 
Zoezi ni full mashaka, nasikia hata hao makarani wenyewe wa NIDA wanafanya kazi bila mkataba. Kuna kila dalili za kuchakachuana kimalipo kwani nimeshasikia minong'ono wengine wakisema wanalipwa kumi japo ilipangwa iwe 15
 
Zoezi ni full mashaka, nasikia hata hao makarani wenyewe wa NIDA wanafanya kazi bila mkataba. Kuna kila dalili za kuchakachuana kimalipo kwani nimeshasikia minong'ono wengine wakisema wanalipwa kumi japo ilipangwa iwe 15
i like ur signature
 
Back
Top Bottom