NIDA sasa kutengeneza vitambulisho kwa miezi 3

NIDA sasa kutengeneza vitambulisho kwa miezi 3

Marwa_J_Merengo

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2018
Posts
4,512
Reaction score
6,882
Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA), imefunga mitambo miwili yenye uwezo wa kuzalisha vitambulisho 9,000 kwa saa ikiwa na uwezo mkubwa zaidi kulinganisha na mitambo iliyokuwepo awali iliyokuwa inazalisha vitambulisho 200 – 250 kwa saa.

Taarifa hiyo imetolewa na kitengo cha mawasiliano na uhifadhi hati NIDA kwa nia ya kufafanua taarifa ya uongo kuwa uwezo wa NIDA kwa sasa ni kuzalisha vitambulisho 1,000 tu kwa siku na kudaiwa kuwa watalazimika kuchukua miaka 82 kuzalisha vitambulisho milioni 51

NIDA imefafanua kuwa vitambulisho milioni 15 vinaweza kuzalishwa kwa kipindi cha miezi mitatu tu kwa kutumia mitambo yake hiyo.

Aidha taarifa hiyo imefafanua kuwa, imewasiliana na mamlaka mbalimbali za Serikali kwaajili ya hatua zaidi na kuanza utozaji tozo na inatambua kuwa kutokana na umuhimu wa mfumo huo, serikali imewekeza kiasi kikubwa cha fedha ili taasisi, wafanyabiashara na wananchi waweze kutumia taarifa za utambulisho kwa shughuli za kijamii.
  • Hivyo imeelezwa kuwa utozaji wa tozo ni moja ya namna ya kurudisha gharama za uwekezaji uliofanywa na Serikali na pia kuwa na mfumo wa utambuzi endelevu.
 
Sisi hatutaki polojo, kama ni kweli watupe vitambulisho vyetu ndani ya muda mfupi,ni mwezi wa nne sasa nasubili changu,njia ya muongo ni fupi.
 
Nina uhakika asilimia 100 kuwa hiyo miezi mitatu itapita na bado watanzania wengi watatkuwa hawajapata vitambulisho. Hakuna siku serikali imewahi kuweka deadline kwenye project yoyote na ikakamilika kwa wakati.
 
Hebu tupeni mrejesho wa hizi porojo, umefikia wapi?
 
kama walikuwa hawana hela wangesema mapema, hata tungelipia Kuna ishu nyingi zinakwama kwa sababu ya hvyo vitambulisho
 
Back
Top Bottom