NIDA: Taasisi iliyofeli kuingiliana na jamii

NIDA: Taasisi iliyofeli kuingiliana na jamii

talentbrain

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2009
Posts
1,187
Reaction score
760
Habari zenu watanzania wenzangu.

Ni Mara ya pili naanzisha Uzi (makala) hapa inayoihusu taasisi hii nyeti imeyopewa mamlaka makubwa na serikali yetu kutupatia vitambulisho vya Taifa. Kwa umuhimu wa vitambulisho hivi ni wazi taasisi hii ni muhimu sana kwa watanzania wote.
Huwezi kupata passport bila kitambulisho hiki, huwezi kusajili kampuni bila kitambulisho hiki na huwezi kusajili laini ya simu bila hiki na huenda hadi December 31 watu wengi wasiweze kusajili laini zao sababu ya uzembe wa taasisi hii.

Hoja yangu kwa leo ni jinsi taasisi hii inavyoendeshwa kienyeji na wasivyoweza kuwa na direct contacts na wananchi wanaohangaika zaidi sasa kuelekea mwisho wa usajili wa laini za simu.

1. Website imekuwa haifunguki kwa siku nyingi sasa. Mwanzo nilidhani ni tatizo la kiufundi ila inaonekana wameshindwa kulitatua. Ukijaribu kifungu website yao haifunguki na kama vile umeishiwa bundle.

2. Wametoa namba nyingi za simu na cha ajabu namba nyingi walizotoa zimefungiwa, hazipo na chachr ziko busy mpaka usiku wa maneno kama vile ziko blocked kupokea incoming calls.

3. Email hazijibiwi kabisa. Kwa experince yangu nimewatumia mails zaidi ya tatu na hawajajibu hata moja ndani ya miezi mitatu.

4. System zao za ndani hazisomani. Nimeenda makao makuu ya NIDA Zanzibar ila haikuweza kusoma details za mikoa ya Kigoma na aidha Kagera mpaka sasa.

5. Online system ya kuangalia namba nayo imekufa tangu website yao iende chini.

Nijuavyo system za serikali ziko chini ya e-government. Ndio kusema serikali nzima ina fail katika hili?

Kama sijasahau taasisi hii ilipewa amri na Rais akiwa Morogoro wahakikishe wanawapatia wananchi vitambulisho. Je, imemaliza huko Morogoro? Na je, juhudi zao zimeishia mkoa huo tu?

Ninaambatanisha na picha ili mthibitishe. Namba zote zilizopo hapa na kwenye mbao za matangazo hazifanyi kazi nk.

ONLINE-ID-ADVERTS-2.jpg


TANGAZO-HUDUMA-YA-SIMU-791x1024-1.jpg


Screenshot_20191220-141131.png
 
Kiukweli nida kwenye hili swala la vitambulisho wamebolonga sana, wametia ugumu zoezi linaonekana lina process kubwa utafikiri unafatilia passport

Saizi ni tuko katika mfumo wa digital wangeweza kurahisisha hili zoezi lifanyike kwa njia ya mtandao kirahisi tu

Kwa mfano zipo fingerprints scanner ambazo mtu angeweza kujisajili hata akiwa nyumbani au sehemu yeyote wanayotoa huduma za internet cafe

Pili vikwazo vimekua vingi, hususani katika kupata hicho cheti cha kuzaliwa. Kero hii ni kubwa sana hususani hapa jijini dar. Haifahamiki gharama elekezi kwa ajili ya kupata hicho cheti, unaweza ukatoa 20k halafu mwingine akapigwa 40k

Mi nishajipanga nimetoa vibuku buku vyangu humu limebakia bundle tu ambalo na stream kwa muda wa wiki tu

Kauli mbiu yetu ambao hatuja register

Wafunge tu
 
Back
Top Bottom