NIDA waje na mpango wa Vitambulisho Kidato cha nne

NIDA waje na mpango wa Vitambulisho Kidato cha nne

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Napendekeza kuwa, NIDA waje na mpango mkakati wa kuwapatia vitambulisho vya NIDA wanafunzi wote wa kidato cha nne wenye sifa.

Kama taarifa zao zitachukuliwa mapema, inamaana kabla ya maliza kidato cha nne wote watakuwa wamepata vitambulisho vyao na kuepuka usumbufu usio kuwa wa lazima.

Tukumbuke kuwa, hili ndilo kundi lenye uhitaji mkubwa na wa haraka wa kupata vitambulisho kuliko wengine kulingana na majukumu yao mtambuka baada ya kidato cha nne.
 
Serikali ya CCM haitaki mawazo ya maana kama haya. Kama mada haihusu kumsifia bi mkubwa, basi kwao ni ubatili mtupu!

Wazo ni zuri sana mkuu!
 
Back
Top Bottom