KERO NIDA wanataka kadi ya kliniki ili kufanya marekebisho ya jina. Mtu aliyekwenda kliniki miaka ya 1990's anatolea wapi kadi hiyo leo?

KERO NIDA wanataka kadi ya kliniki ili kufanya marekebisho ya jina. Mtu aliyekwenda kliniki miaka ya 1990's anatolea wapi kadi hiyo leo?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Joshua Simon

Member
Joined
Oct 29, 2016
Posts
6
Reaction score
4
Mke wangu ana changamoto ya kutofautiana majina kati ya kitambulisho cha NIDA na vyeti vyake vya kitaaluma.

Nimejaribu kufuatilia vigezo vinavyohitajika Ili kufanya marekebisho, nikakuta pamoja na vigezo vingine ni pamoja na KADI YA KLINIKI.

Sasa hapa kweli, mtu aliacha kwenda klinic miaka ya tisini na huko, leo anatoa wapi kadi?

Na kuna msisitizo kuwa, endapo ukikosa nyaraka mojawapo hapo ombi lako halitashughulikiwa.

Hii kwangu ni kero kubwa sana.

Soma Pia: Waziri Masauni: NIDA kuna shida ya usimamizi, Uongozi una shida, Watu wanateseka kupata Vitambulisho

Nida.jpg
 
Back
Top Bottom