MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa ( NIDA) wametoa msaada wa mahitaji maalumu ikiwemo vyakula kwenye kituo cha watoto Kurasini jijini Dar es salaam lengo likiwa ni kusherehekea kuelekea sikukuu ya Eid al-Fitrna Pasaka.
Akizungumza leo Machi 29, kwa niaba ya Mkurugenzi wa NIDA, Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi, Shariff Fadhili amesema mamlaka imetoa msaada huo ikiwa ni kurejesha kwa jamii kwani pia wao ni wateja wao na wanapaswa kukumbukwa kwenye kila kipindi.