Nidhamu katika uongozi

Nidhamu katika uongozi

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Posts
608
Reaction score
1,655
Ni muhimu kurudia hii mada mara kwa mara ili iingie akililini mwa watu kuhusu nidhamu katika uongozi na jinsi gani huleta mwelekeo kwa watu unaowaongoza kama wewe mwenyewe kiongozi una nidhamu.

Nidhamu ni uwezo wa akili ku control matendo na maneno na kuelekeza matendo na mawazo katika mkondo sahihi ambao utakuwa na manufaa ya kiakili, kiroho , kimwili pamoja na ki mali. Kwasababu ili binadamu akamilike na awe mwenye afya njema ni lazima awe na siha ya vitu vyote hivyo.

Matendo mengi binadamu anayofanya mabaya inatokana na kukosa nidhamu ya kufuata na kutenda kilicho sahihi ama pengine kutokujali kuangalia hatua anazopiga kama ni sahihi au sio sahihi kwa kufuata njia ya mkato katika maendeleo wakati huo huo akiacha akili yake ikiwa haijakomaa na kuharibu nafsi yake na ya jamii yake kwa ujamla kwa uovu.

Ni muhimu kabla kufanya kila tuangalie jamii kwanza itafaidikaje kabla ya kujiangalia wenyewe, kwasababu maendeleo mazuri ni yale ambayo jamii kwa pamoja inapiga hatua.

Mara nyingi disorder katika akili ya binadamu hupelekea disorder katika jamii kama physical manifestation of the spirit. Ni muhimu sana ku control mawazo yetu na kuyaelekeza katika wema ili taifa letu liendelee na sio injustice na selfishness. Ni muhimu kwahiyo kuwa na umoja wa kiakili na ni muhimu kuelekeza mawazo yetu katika wema na faida ya pamoja ya jamii na sio faida binafsi ya watu.

Hatutaweza kujenga taifa hili vizuri likawa na order kama hatutazingatia mambo haya ya msingi ambayo mizizi yake lazima ijengwe katika kila roho ya mwananchi.

Kwahiyo kiongozi lazima awe na nidhamu awe na uwezo wa kudirect mawazo yake katika mkondo unaofaa ambao ni productive awe na uwezo wa kudhibiti matendo yake na mdomo wake dhidi ya utengano katika nchi.

Sisi ni ndugu ni watu wa taifa moja ni lazima tupendane ili tujenge taifa moja kwakuwa bila kuwa wamoja na bila kupendana hatutaweza kujenga misingi imara ya taifa hili.

Taifa lolote lile ambalo misingi yake ni fedha na ambalo haliangalii kwa ukaribu mahusiano ya watu wake, bali akili na roho zimeelekezwa katika fedha, halina furaha. halina umoja. Migogoro haitaisha na chuki itakuwepo. Watu watagombania uongozi sababu ya fedha na sio maslahi mapana na wema wa jamii nzima. Maadili ya jamii yatashuka kwa kiwango kikubwa na nidhamu na kujizuia kutawekwa pembeni. Raia wake watapenda raha kuliko utu na umoja wao. Tutakuwa na viongozi wapenda raha na starehe , wala rushwa na mafisadi hawatajali jamii tena bali maslahi binafsi na starehe. Katika mazingira haya haki haiwezi kusimamiwa.

Watu watataka uongozi sababu tu ya madaraka na mali lakini sio haki za raia, wema na maendeleo ya pamoja ya jamii. Wataingia madarakani kupitia kitu kinachoitwa demokrasia kwa kuwadanganya wananchi na kusababisha vurugu na fujo sababu ya uchu na ubinafsi.

Kwasababu wamekosa nidhamu ya kudhibiti tamaa na uchu wao kwa manufaa ya umma. Wataleta confusion katika jamii na sio leadership kwasababu uongozi ni kuipeleka jamii sehemu inayostahili katika wema, kuibua wema katika kila nafsi ya raia kuutenda wema huo kwa raia mwenzake, kuitumikia nchi na kutumikiana kama raia wa nchi moja na sio maadui. Na juu ya yote kuhimizana kupendana kama raia wa nchi moja.

Kama kiongozi anashindwa ku control mdomo wake na matendo yake na kuelekeza mkondo wa mawazo yake na matendo yake katika njia sahihi hafai kuwa kiongozi. Kiongozi lazima awe mfano kwa jamii na kwa familia yake. Ni lazima tuangalie anavyoendesha maisha yake katika jamii na katika nyumba yake mwenyewe. Je anaheshimu nyumba yake? Anaishije na jamii inayomzunguka ? Watoto wake wana adabu? Kwasababu kama kiongozi akishindwa ku control nyumba yake atawezaje taifa?? Kama akishindwa kuiweka nyumba yake katika good order atawezaje taifa?

Kwahiyo ndugu zangu nidhamu huleta dira iwe kwa mtu binafsi au taifa na ni kionjo muhimu sana katika uongozi. Nidhamu ni good ordering of the mind. Ni muhimu kwa kiongozi kuwa na nidhamu nchi haiwezi kuwa na order kama viongozi hawana nidhamu. Lakini pia pasipo nidhamu ni ngumu kupata maendeleo kama taifa. Ikiwa viongozi na raia hawana nidhamu. Nidhamu huleta dira.

We must do what is just, right and fair, to our country and our country men. Tunajidanganya tunapochukua rushwa na tunapofanya ufisadi tunaliua taifa letu wenyewe. Umoja wetu na mshikamano wetu unaondoka na upendo wetu kwa binadamu wenzetu unatoweka sababu ya hivi vitu.

Ni lazima tutende wema na tufuate kilicho chema ili tuwe na afya ya kiakili na kiroho. Tutendeane haki na tufuate mkondo ulio sahihi ndipo nchi yetu itakapo ponywa. We must do good.
 
Back
Top Bottom