Nidhamu Kwa wachezaji yamtimua Amunike?

Nidhamu Kwa wachezaji yamtimua Amunike?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Hakuna ubishi Amunike na Zahera walikuwa hawana mzaha kuhusu nidhamu ya mchezaji ndani na nje ya uwanja.

Simba hawakuwa vizuri na Amunike alivyowaadhibu wachezaji wa Simba walipochelewa kuripoti kambi ya mazoezi. Simba pia walimind Amunike alivyoacha kuwachezesha wachezaji wa Simba Shabalala na mwenzake Nyoni kule Afcon.

Inafahamika kuwa TFF ina viongozi ambao ni wapenzi lialia wa Simba. Hii inaweza kuwa sehemu ya uwamuzi wa kumfukuza Amunike.

TFF haitaki kuhusianisha matokeo ya taifa stars iliyoyapata na
1. Maandalizi mabaya ya timu
2. Budget ndogo ya taifa stars
3. Ligi yetu kujazwa wachezaji wa kigeni
4. Uwezo wa wachezaji wetu kulinganisha na wachezaji wa timu pinzani ambao wengi wao Wana exposure kubwa
5. Ligi yetu mbovu ambayo hata ratiba haieleweki
6. Ligi inayochezeshwa na marefrees ambao wanaidai TFF
7. Madai ya kocha ambaye anaidai TFF
 
Wakawe walimu wa nidhamu Soka hawaliwezi
 
Sawa Dr. tumekupata.
Hivi Kwa akili zenu taifa stars ingeweza kuifunga timu gani pale kwenye lile kundi lao? Kila timu pale ilikuwa ina mchezaji wa EPL sisi hatuna hata mmoja. Algeria na Senegal zote zimeingia nusu final, inaonyesha hazikuwa timu za kufungwa na taifa stars. Amunike arejeshwe haraka kaonewa na wakora
 
Back
Top Bottom