Nielesheni mwezi mrefu na mfupi wa Hedhi

Nielesheni mwezi mrefu na mfupi wa Hedhi

Machuchu

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2017
Posts
1,260
Reaction score
965
Mwezi mrefu na mfupi huwa sijuagi...nimejalibu kufuatilia kwa makini kwa mfululizo ndani ya miezi mi3 ili nijue kama ifuatavyo:-

August nimeanza tarehe 23
September nimeanza tarehe 20
October nimeanza tarehe 18
Je, apo mwezi wangu kwa ujumla utakuwa mrefu au mfupi?
Je, tarehe za hatari zitakuwa kuanzia siku ipi
Je, siku zangu salama ambazo siwezi pata ujauzito itakuwa siku ya ngapi? ni hayo tu

Naomba msinibeze au kunitusi nimeuliza kwa kua sijui nilijualo. Nawatakia siku njema.
 
Ni rahisi....
1.hesabu kuanzia tarehe 23august mpaka tarehe 20september ni siku ngapi andika pembeni
2.hesabu kuanzia tarehe20 september hadi 18 october ni siku ngapi

Ukishafanya hivyo uje unipe majibu nikutajie siku salama na hatari
 
Anza kuhesabu siku ya kwanza unayoona damu ya hedhi mpaka siku ya mwisho kabla hujaanza mzunguko mwingine. Mfano, hesabu kuanzia August 23 mpaka Sept 19 utapata siku 28, halafu hesabu kuanzia Sept 20 mpaka Oct 17 utapata siku 28 kwahiyo mzunguko wako ni wa siku 28 ambao ni wa wastan.Kwa mzunguko wa siku28 siku za hatari ni kuanzia siku ya 10 mpaka siku ya 18. Kuna baadhi ya wanawake hupata dalili kipindi yai linapotoka (ovulation period) kama kuumwa kiuno au nyonga upande mmoja au zote,kuhisi kichefuchefu,hamu ya tendo la ndoa kuongezeka, joto la mwili kuongezeka na kutokwa na majimaji ya kuteleza kama mlenda sehemu za siri. Jaribu kufatalia hizo dalili ili ujue ni wakati upi yai linatoka, kwa mzunguko wako(siku28) huwa siku ya 14 au 15.Ingia google play store download app ya period tracker itakusaidia zaidi hutapata shida.
 
Aisee iyo picha ya avatar yako ni wew kweli? Duh
 
Kumbe hili somo la kujuwa siku za hatari na salama kwa wanawake wengi bado ni somo gumu sana.
Ndio maana masingle mom wanaongezeka daily
 
Hivi ikitokea ukawa mjasiriamali ukawa unaikusanya hiyo damu kama raw material akina dada watapiga hela sana na wataacha kuomba omba hela
 
Hivi ikitokea ukawa mjasiriamali ukawa unaikusanya hiyo damu kama raw material akina dada watapiga hela sana na wataacha kuomba omba hela
Mkuu naskia damu ya hedhi ni kitu cha kukimbiwa. Sasa sijui atapiga dili vip.[emoji20]nimethink twice
 
Siku salama..siku ya 11 hadi ya 17 wastani.
Au siku ya 10 hadi ya 18 Kama alivyosema dada Alliyah hapo juu.
Hili ndo la muhimu zaidi kujua.
N.B siku ya kwanza Ni ile uliyoanza period.
 
Being a singleparent haihusiani kabisa na kalenda
Hivi kama mwanamke ajui siku zake za hatari alafu akasex na jamaa ambae awana malengo ya kuoana alafu huyo binti akapata mimba unafkiri huyo jamaa atakubali kumuoa huyo binti kisa tu amempa mimba
 
Na mwenye mzunguko wa siku 18 je huyu anakua kundi gani? siku zake za hatari na salama ni zipi? je ana uwezo wa kubeba mimba?
 
Back
Top Bottom