Poleni Shadya na Preta...nikuwa nakula ugali kwa dagaa for lunch, mtamu balaa!
Shadya, ni vigumu kidogo kujua urefu wa mwezi kwa kutoa trend ya mwezi mmoja tu, kwani huwa cyle inabadilika badilika kwa siku moja mbili hivi. Tarehe 26 September mpaka 24 October ni siku 27 hivi...naamini mzunguko wako utakuwa wa siku 28. Tuanzie hapo...
Unaanza kuhesabu tangu siku umeanza ingia hedhi...hivyo tutaanzia tarehe 24. Kwa mzunguko wa siku 28, ina maaka siku ya kati kati ya mzunguko ambapo yai linatolewa (ovulation) ni siku ya 14. Kwahiyo ukiongeza siku 14 kwenye tarehe 24 tunapata tarehe 6 ya mwezi november kuwa ndio siku utatoa yai.
Lakini yai linaweza rutubishwa na mbegu zilizomwagwa ukeni hata siku zilizopita kabla ya yai kutoka, na pia mpaka siku 4 tangu yai litoke...so siku zako za hatari zitaanzia tarehe 3 November mpaka tarehe 10 November. Siku ambazo zina uwezekano mkubwa wa kuzaa mtoto wa kike ni tarehe 3, 4, na 5 November...na siku za uwezekano mkubwa wa kuzaa mtoto wa kiume ni tarehe 8 au 9 November.