Nifanyaje ili mchuzi uwe mzito

rasai

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2013
Posts
230
Reaction score
341
Habari,

Jamani mwenzenu naomba kujuzwa nifanyeje ili ninapo pika mchuzi uwe mzito, na kuwa wa rangi iliyokooza, inakaribia black. msaada please

 
Ngoja watalaamu wa mapishi waje, though mchuzi unahitaji viungo na vikolombozwe vya hapa na pale ili uwe mzito
 
Unataka uzito wa kiasi gani?

Anyway weka karai lenye mafuta, kaanga vitunguu km unavyofanya kwa chips. Zikiwa golden brown zitowe weka pembeni kuchuja mafuta, yasiwe kidogo sana.

Kwenye blender weka tungule na tomato paste kiasi unachotaka saga. Kaanga mchuzi km kawsida utaweka na hivo vitu hapo, hivi viwili vikifanyika utapata mchuzi mzito na uliokoza.

kwa ladha zaidi usiache kuweka kotmiri.
 
shukran, nmekupata vilivyo. natumai sasa ntaupatia huu upishi. asante sana
 
shukran, nmekupata vilivyo. natumai sasa ntaupatia huu upishi. asante sana

Usisahau karoti ilokwanguliwa....nayo inafanya mchuzi uwe mzito mzito.
 
Mchuzi unapendeza ukiwa na rangi nyekundu ama orange flan hivi sasa hiyo nyeusi hapana kwa mm lakini.
 
Mwiko wa upishi wote, ni kuunguza kitunguu ama undercooking it. Kitunguu kinakaangwa hadi kuwa brown.

japo sijaelewa,mchuzi unamaanisha stew ama sauce?
 
Mwiko wa upishi wote, ni kuunguza kitunguu ama undercooking it. Kitunguu kinakaangwa hadi kuwa brown.

japo sijaelewa,mchuzi unamaanisha stew ama sauce?
asante namaanisha rost lakulia wali.
 
Mchuzi unapendeza ukiwa
na rangi nyekundu ama orange flan hivi sasa hiyo nyeusi hapana kwa mm
lakini.

kweli red na orange nzuri, nakumbuka mama hupika wa njano pia.
 
kuna options kadhaa huwa natumia depending na aina ya chakula,unaweza tumia royco mchuzi mix ila jihadhari usieke chumvi nyingi.mana yenyewe huwa ina chumvi,au koroga unga wa ngano kiasi afu mix kwenye mchuzi,njia ingine ni kuacha chakula kiive sana vitu km ndizi na viazi.vinalainika vinafanya mchuzi mzito...ingine kama ni tomato soup plain unaweza pika huo mchuzi ukaiva afu ukasaga kwenye blender na kiazi ulaya kilichochemshwa tiari,chuzi lazma liwe zito...pia kuongeza ladha unaweza unga mchuzi na vitunguu saumu au tumia curry powder mi huwa.naipenda harufu yake
 
Sante, nmekupata. Hii ya kueka ngano, nlipata muona dadaangu mmoja akieka maharage yawe mazito, ila yalikua ya biashara. Skupata tumia kwa mchuzi, nashkuru kwa maarifa
 
Sante, nmekupata. Hii ya kueka ngano, nlipata muona dadaangu mmoja akieka maharage yawe mazito, ila yalikua ya biashara. Skupata tumia kwa mchuzi, nashkuru kwa maarifa
ur welcomed dear...
 
usibanie viungo na usijaze mimaji,hilo la black unaweza kuviivisha sana vitunguu
 


Tungule mchuzi unakuwa mchungu ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…