Nifanyaje ili niokoke?

Mbavu za Mbwa

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2011
Posts
303
Reaction score
154
Wana bodi! Ni hadithi ndefu sana, ila kwa ufupi wake ni kuwa mtumishi mwenzangu tunaefanya kazi ofisi moja na desk moja amemuweka kimada aliyekuwa mpenzi wangu kwa miaka 4 na ofisi nzima wanamjua. Nilijaribu kumsihi huyu jamaa kuwa asitishe uhusiano wao kwa kuwa unaweza kutuvuruga, hakukubali. Simuonei wivu kabisa, hofu yangu ni kuwa; Je, hakuna uwezekano wa kujengeka uadui kati yangu na huyu jamaa? Ukizingatia, nyumba wanayoishi ndipo kuna duka langu na huwa nakuwepo hapo dukani(nyumban kwao) muda wote nikitoka kazin na siku za weekend. Mbaya zaidi mwanamke huyo amekuwa akinipigia simu na kuni-sms kuwa mimi ni mtu muhimu sana kwake na kamwe hawezi kukata mawasiliano nami. Nimekuwa sipokei simu wala kujibu msg zake. Nikibadili namba za simu, anazitafuta. Naomba ushauri, nitaepukaje janga hili? Maana hata dukan kwangu nakuwa sina amani pindi akija kununua vitu, naogopa huyo bwana wake akimuona dukan si atahisi bado tu wapenzi? Na uwezo wa kutafuta eneo lingine nihamishe duka sina. NISHAURINI NDUGU ZANGU.
 
Kwa nini unashindwa kuhamisha duka? Kwani hapo ni bure?
Well, get a grip aisee! Mwanaume mzima unashindwa kumkazia sauti huyo dada na kumuuliza 'unasemaje?' Anapokupigia simu? Uko weak kiasi hicho? Aisee..
 

"...mwana wa mtu kizuka, akizuka zuka nae!"
 

Yaani unakubali kukejeliwa kwa lipi? Kuwa mwanaume maana yake ni kuwa na misimamo. Mwambie huyo mwanamke kuwa hupendi makahaba siku hizi
 
Wewe achana na huyo mwanaume, mana anafahamu kuwa ulikuwa na uhusiano na huyo mwanamke toka mwanzo.

Kuna wanaume wengine aisay wala hawana noma, hata kama mke wake anapigwa nje.....Yani nilikuwa naona lo fa mmoja mke wake anachukuliwa hasa, hata ikafikia wanamwambia mmke wako anakwenda nje yeye anasema wanamzulia tu.

Nashaka huyo mwanaume ndo wale hata mke wake akikaangwa nje anasema wanamzulia tu.

Kuepukana na huyo mwanamke ni kazi ndogo sana mwambie siku hizi una majini, hayapendi wanawake na mwanamke anaye mfata basi majini yake yatamtesa.

Na wanawake walivyo waogo, basi atakukacha tu hata sogea tena :biggrin:
 
Inatakiwa tufike wakati tukue!Kwanini unahofia usichokijua?Kuna uadui gani rafiki yako kuwa na uhusiano na ex wako?
 
huyo mwanamke mfungie vioo mazima. Tena mwambie Akiendelea kukutext utamwonyesha jamaa yake hizo text.
 
Nilidhani mambo ya maana, loooh, kumbe ujinga mtupu!
 
..maamuzi mepesi kwake magumu na magumu itakuwaje....!
 
Huwezi shindwa kufanya kazi zako kisa wao wanaishi karibu na dukani kwako wewe fanya mambo yako kama kawaida na akija dukani una kuhudumia kama mtejamwingine yoyote yule wa kawaida na si vinginevyo usimwongezee kitu wala kumpunguzia, ila kwa upande mwingine usi endekeze hiyo tabia ya mawasiliano anayotaka kuianzisha kwani ni rahisi kuibua hisia hasi. Kuwa na msimamo mmoja fanya shughuli zako wewe na yeye imebaki zilipendwa.
 

Hadithi za kutunga utazijua tu.
Kwanini uliachana naye huku unamshauri work mate wako aachane naye simply atawagombanisha.!!!!
 
wewe natahani ni wa kiume,kaza uso kaka,u r so weak!!!
 
Acha Udhaifu, ukina hafai wenzako wanajiuliza watampata lini. Hivyo Kama Kweli Wewe ni Mtu Mwenye Msimamo wako hauwezi kuzuia mwanzako kumchukua demu wako mliyeachana naye, huo mpango wa kuona demu anafaa baada ya kuchukuliwa na mwingine ni umasikini wa mawazo ambao unafarijiwa na ule usemi kuwa demu anakuona wewe ni muhimu kwake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…