SAUTI YAKO
JF-Expert Member
- Jan 25, 2014
- 2,944
- 2,032
Asante kwa ushaur ntautendea kaziMkuu nunua carton ya maji ndogo hata elfu 5 haiishi kwenye maduka ya juml,a hakikisha mtoto anatumia maji hayo tu...Kama unamuacha nyumbani na housegirl hapo ndo kuna changamoto ya kuhakikisha anampa mtoto hayo maji na si mengine...Mi nipo kwenye mkoa ambao hakuna tatizo la meno kuharibiwa na maji ya kunywa ila kwa ajili ya kuepuka matatizo yanayoletwa na kunywa maji yasiochemshwa huwa nanunua carton hizo kwa ajili ya watoto wangu na kila asubuhi kama anaenda shule lazima aende na maji ndogo....Imesaidia saidia kuepuka magonjwa ya matumbo kwa watoto wangu...
Niko katika mkoa ambayo wakazi wake meno yamebadilika rangi kutokana na maji wanayokunywa.
Mimi nilihamia huku nilipo mwaka jana na mwanangu mwenye umri wa mwaka mmoja hajazaliwa huku alikuja hapa nilipo akiwa tayari ana mwaka mmoja.
Lakini tangu afike nimekuwa nikimpa maji haya ya bomba wanayokunywa wenyeji, je wakuu siku za usonI haiwezi kufanya meno yake yabadili rangi.
Naomben ushauri maana mkoa nilipo nipo kwa muda wamiaka 5 tu natarajia baada ya kipindi hicho kupita nihame sitaki mwanangu tutapohama awe hivyo, je niwe namnulia maij ya chupa au nifanyaje.