Nifanyaje nipende tena

The Lost Boy

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2020
Posts
248
Reaction score
311
Kuna binti nilimpenda mno wakati nipo shuleni. Mimi nikiwa form five yeye yupo form two. Kipindi hicho sikuwahi mwambia hisia zangu kwani nilimuona kama mtoto bado, nikahisi ningemvuruga kiakili kumuambia mambo ya mapenzi.

Nikahitimu form six na kujiunga na chuo yeye nikimwacha shuleni. Tukapoteza mda mrefu sana.

Baada ya kitambo hicho mwaka 2021 nikapata mawasiliano yake kupitia kwa jamaa yangu. Nikamtafuta. Tukaanza kuwasiliana mara kwa mara. Kutakiana siku njema, usiku mwema, karibu chakula nk. Chombeza Chombeza hizi ndio hisia zile za zamani zikafufuka tena. Sikutaka kupoteza muda nikamuelezea hisia zangu juu yake ambapo alikubali tuwe na uhusiano.

Nilikuwa yule yule. Nilimpenda mno. Mno yani. Hata nashindwa kuelezea. Hakuhitaji kitu nikashindwa mpatia. Upendo nilioanza nikiwa mtu mzima ninayejitambua.

Upande wake bint ilinidhihirikia wazi kuwa hakunipenda kihivyo, ila nilijipa moyo kuwa huenda upendo utaongezeka kadri siku zitavyokwenda.

Kipindi hicho jamaa zangu wengi walikuwa wanaoa. Binti huyu nami nikaona ananifaa kabisa. Basi baada ya uhusiano wa muda mfupi nikamshawishi nipeleke posa kwao, ambapo alikubali. Nikaongea na wazee wangu, posa kweli ikapelekwa.

Sasa siku wazee wanaenda kufata majibu ya posa, nikiwa natumaini makubwa ghafla jioni moja binti akanitumia sms ndefu akiniarifu kuwa anaomba uhusiano wetu uishe kwani tayari ana mtu mwingine moyoni mwake kabla yangu na hawezi kumuacha. Akaniomba radhi kwa kutonijuza mapema. Lawama za hapa na pale bado alisimamia pale pale

Mda huo nilikuwa nimeshawatangazia jamaa zangu kuwa waandae michango nipo kwenye hatua za mwisho za kujitwalia jiko. Bimkubwa pia alikuwa ashaanza kuwaambia marafiki zake juu ya hili.

Upande wa wazazi wa binti walikuwa wamekubali na kuridhia kabisa, binti ndio alikuja kukengeuka

Sikuwa namna bali kukubali hali halisia. Sikutaka kulazimisha penzi.upande wa wazee nikatufuta sababu za uongo nikwaambia, mwisho nikaahirisha ile posa. Wazee wakakubali

Moyo wangu uliumia baada ya hili tukio. Nilijikuta nimeanza kutumia madawa ya kulevya kwa maana hata usingizi nilikuwa nakosa. maumivu moyo yalikuwa makali mno kwangu. Huu ulikuwa uhusiano wangu wakwanza nikiwa najitambua

Baada ya muda mrefu kupita niliweza kurudi katika hali yangu ya kawaida na madawa nakaacha

Sasa shida ni kuwa ni mwaka wa nne sasa nashindwa kupenda tena. naona ni hali ya Kawaida tu kuwa single. Wadogo zangu wanaoa kila siku ila mim sina habari na wala hainitatizi. Sina hamu kabisa na uhusiano. Nifanyaje nipende tena maana siku kusogea.
 
Pole sana mkuu, nadhani alichokosea huyo binti ni kutokukwambia mapema, japo uamuzi wa kukwambia ni mzuri sana na nadhani kama ungeingia kwenye ndoa nae, yangekukuta zaidi ya hayo.

Kuhusu kupenda tena, huo ni uamuzi wako. Inabidi ukubaliane na hali kwamba yule ameshaondoka, na past yako haiwezi kuharibu future. Najua wapo girls wengi karibu yako, jaribu kuufungua moyo wako. Ruhusu mtu aingie, hata kwa urafiki tu. Moyo una kawaida ya kupambania kitu unachotaka, so ukiwa na mtu karibu ni rahisi moyo kufunguka.

Nje ya mada, huyo binti aliyekutosa muda wa kupeleka posa, Yuko wapi now?
 
mh! akili yangu inayotafunaga bangi badala yakuvuta inaniambia lengo la uzi sio mapenzi ni jengine kabisa!.. sijui mmenielewa!
 
Unamuitaji Yesu tu nenda kanisani kama uko dar nendakwa pastor katunzi kwa maombi na ibada hapo utabadilika sana kumbuka si kila kanisa ni la Yesunila kwa pastor katunzi kuna Yesu kwelikweli...
 
Hutakiwi kuoa mwanamke unayempenda hii formula Kwa wanaume tu ukimpenda mwanamke wafa mapema sna , oa mke anayekupenda maana mwanamke anapenda ila anachangamoto ya kutii ndiyo maana Sheria inamtaka atii, mwanaume anatakiwa apende maana hiyo ni changamoto kwake utii Kwa mwanaume ni kawaida yake vitabu vya dini vyabainisha hivyo

Mie nachokua ni moto mbele Kwa mbele tu
 
Mwanaume haina haja ya kupenda ni kujitafutia matatizo tu , wewe tafuta manzi mrembo anaekuvutia kimapenzi na wife material kisha muoe maswala ya kupenda waachie wanawake , wewe penda hela.
Halafu acha Nyeto inakutia Uzege
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…