Nifanye nini jamaa fulani ni msanii mzuri nataka kumtoa aonyeshe kipaji chake?

Nifanye nini jamaa fulani ni msanii mzuri nataka kumtoa aonyeshe kipaji chake?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Kuna braza mmoja ni mwanamziki ila yeye anatumia gitaa lake la asili katengeneza Kwa kutumia fimbo, waya na kikopo ila ukisikiliza sound yake ni quality sana.

Jamaa huwa anajitolea kuburudisha akiwakuta mmekaa kijiweni anaanza kupiga mziki na mashahiri yake tuseme anaimba kama remmy ongala Hivi.

Sasa nimeona anafanya kitu kwa moyo na kwa muda mrefu sasa hajapata nafasi ya kuonyesha alichonacho ili Dunia imuuone imfuatilie.. Nachotaka ni kujua tu dondoo za kumtangaza sikutaka kuweka vipande vyake hapa nataka iwe maalum iwe surprise ndo maana nikawaza lazima tupate camera kali ili nimrekodi niwe kama meneja wake una lipi la kunishauri kuhusu kuitangaza content ya Jamaa.

Nguvu ya mitandao ni muhimu je nimsaidie vipi namna ya kujiunga au mitandao gani nimsajilie maana hata simu hana.. Awe msanii rasmi na Haki zake zilindwe.. Ni post video ngapi angalau Kwa week nipeni hints za kuweza ku mtrendisha akitoboa yeye na mimi si itakuwa nimetoboa.
 
IMG-20240626-WA1385.jpg
 
Back
Top Bottom