Nifanye nini katika hali hii??????

kaka duniani kuna matatizo sana ila maji yakishamwagika hayazoleki mshauri huyo binti cha kufanya kisheria kwa kuwa amezalishwa hayo mengine yakukaa miaka 11 unamsubiri sio issue kabisa ktk dunia ya mapenzi watu wanaacha wake zao walioishi nao na kuzaa watoto kibao tena baada ya kulipwa mafao ya uzeeni sembuse huyo mwenye mtoto mmoja tu

naendelea kukushauri achana nao hao watu utaumiza kichwa bure na hautasaidia kwa chochote kama vp mtunze huyo mtoto wa ndg yako kama unamwonea huruma ila sio unaanza kumtafuta huyo dogo wakati ameshaoa na anaendeleza maisha yake na mkewe. Husiingile sana mambo ya watu utakufa bure siku si zako kwa presha ya kujitakia
 
nilikua nasisitizia tu hapo kaka angu yaani nini funza yeyote ajiweke kwenye nafasi ya huyo dada halafu apime maumivu yake
imeshatokea sasa utafanyaje inabidi tu akubali matokea na asonge mbele. Hii ndio uwa inadumaza w/wake tatizo likitokea mtu anashindwa kulikabili na kuishia kuudhunika maisha yote wakati kumbe angeweza kuli-handle na kulitupa kule na kupiga moyo konde ili kuendelea na maisha
 

Its sad men. Take time. Yana mwiso..:redfaces:
 


Waungwana Japo kazi bado pevu, NINA KILA SABABU YA KUWASHUKURU WANA JF mliotoa mawazo yenu juu ya nini nifanye kuhusiana na suala zima la dogo kama nilivyoandika hapa chini.
Baada ya kumtext dogo na kumwambia tunaheshimu uamuzi wake na niko tayari kumsikiliza na kumuelewa bila kumu-offend amenitafuta na nimeongea nae kwa muda mrefu sana.


Alichoniambia ni kwamba alifanya uamuzi huo binafsi kwani alifikia mahali kutambua kuwa hawezi kukaa nae tena na lijiona kumpenda zaidi huyu mwingine waliesoma nae chuo.
Ukweli ni kwamba dogo is like he doesn't care juu ya mwenzake aliemuacha mwanza. Ni kama anacheza mchezo Fulani wa kuigiza mpaka nikahisi au HILI TOTO LIMELOGWA NINI. Eti ananiambia alishindwa tu kumuacha na kumwambia hamtaki kwa sababu tayari alishampa mimba na hivyo amekubaliana na mke wake mpya kuwa aendelee kukaa nae kwa muda mpaka apone kidonda kasha amuambie kuwa ameoa mwanamke mwingine na hivyo hana mpango wa kukaa nae ila amuachie tu mtoto aendelee kutunza yeye akaendelee na mipango mingine ya maisha.



Pia anasema aliamua kutokututaarifu sisi wala wazazi wake kwa sababu anasema tungemtibulia na mpango wake ni kuwa mwanzoni mwa mwezi ujao ndio ataweka wazi kwa kila mtu juu ya uamuzi wake. Mawazo yake itakuwa siri kama anavyotaka kichwani mwaka huku akisahau kuwa mama yake yuko kwenye constant contact na wazazi wa binti. Ndo maana nasema limelogwa hili toto.

Kwa ushauri wenu nimeonelea nimtume tu wife week hii akamchukue toka Mwanza aje tuishi nae kwa muda huu. Dogo nimemwambia kuwa atampigia simu na kumtaarifu kuwa amwambie binti aambatane nasi kasha anipe jibu kama amekubali ili wife ndio akamchukue.


 

Ahsante kwa mchango wako. Ni mchango mzuri sana.

But you do not know the cost of being a responsible minded person. Mchango huu ni wa muhimu na unaweza kusaidia wengine katika mazingira yao, ila kwa mazingira niliyopo na hali halisi i cant afford doing what you ask me to.

Hope umenielewa vizuri, this is a matter of someones life and making myself irresponsible i can count as one of my greatest failures in life.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…