Nifanye Nini kutimiza hili wazo la biashara na sina mtaji wa kuanza nao?

Shozylin

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2022
Posts
341
Reaction score
699
Wakuu habari za mida hii.?

Naamini kuna nguvu ya mapinduzi kutoka kwenye mawazo za watu (ideas)

"Wazo" Mungu akasema na tumfanye mtu kwa sura na mfano wetu " vyote tuvionavyo vimetokana na mawazo ya Watu.

Wewe hua unafanya Nini pale unapo kua na idea flan kubwa ya biashara na ukashindwa kutimiza kutokana na kukosa mtaji wezeshi.?

Kwa upande wangu hapa idea yangu si ngeni inafanywa na watu na baadhi yao wamejaribu sjui matokeo yao.

Kwa upande wangu nimewaza namna ya kuiendesha kwa utofauti kidogo.

Bahati mbaya ili idea hii itimie inahitaji taaruma ya mtu (IT) nami Sina mtaji

Ipo hivi idea yangu ni kutengeneza application ya uuzaji na ununuzi wa bidhaa "online" naskia kuna jamaa hapa tz aliwahi kutengeneza yake inaitwa "kupatana"

Sasa idea yangu inafanana na hii ila mbinu za uendeshaji hapa ndipo tutakapo tofautiana.

Vifaa vinavyo hitajika ni laptop yenye uwezo wa kusave data pamona na gharama ya utengenezeji wa hii application.

Ila hapa nilipo Sina pesa ya kutosha kuwezesha hili wazo langu liwe katika uharisia. Nifanyeje ili litimie.?

Nakaribisha mutu aje aje nishee naye hii idea akiona inafaa tuifanyie kazi.
 
Wazo zuri ningeweza kukusaidia kudevelop toka chini kabisa (from scratch) ila bora ufikirie kitu kingine ninavyowajua wabongo ndio shida ilipo anyway tunaweza tumia WordPress na freehost ya infinityfree kwakua hauna mtaji
Mkuu kwanini nifikirie kitu kingine.?
 
Wazo zuri ningeweza kukusaidia kudevelop toka chini kabisa (from scratch) ila bora ufikirie kitu kingine ninavyowajua wabongo ndio shida ilipo anyway tunaweza tumia WordPress na freehost ya infinityfree kwakua hauna mtaji
Kaka Unaweza Kuni PM Contact Tuwasiliane Kuhusu Suala La YetuTalk
 
Ipo hivi idea yangu ni kutengeneza application ya uuzaji na ununuzi wa bidhaa "online" naskia kuna jamaa hapa tz aliwahi kutengeneza yake inaitwa "kupatana"
1. Hii sio "idea yako" ni ideas ambazo zilisha fanyiwa kazi , kilichobakia ni wewe ku copy ,kuboresha kwa kuongeza au kupunguza baadhi ya vitu .

2. Kuna tofauti kati ya classified ads app(matangazo) na "online purchasing app"
Mfano app kama jiji, kupatana (uliyoitolea mfano), hizi ni classified ads app - ni app za matangazo ya biashara, bidhaa na huduma , lakini sio app za "kununua wala kuuza"

Na ndio maaana unaona haufanyi malipo yoyote, wala transaction kulipia bidhaa huko!

3. Mfano wa app za kununua na kuuza ni kama: inalipa , aliexpress etc, hizo ni qpp ambazo unaweza lipia na kununua bidhaa direct
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…