Nifanyeje ili niweze kutuma maombi ya ajira Serikalini?

Nifanyeje ili niweze kutuma maombi ya ajira Serikalini?

benwise

Member
Joined
Oct 24, 2015
Posts
99
Reaction score
75
Salam wakuu.kuna ndugu yangu amehitimu chuo cha ualimu kwa level ya shule za msingi miaka mitatu iliyopita na sasa kwa zaidi ya miaka miwili anajitolea kwenye shule fulani huo mkoani.

Changamoto iliyopo tangu ajira zimetangazwa mara ya kwanza na hata sasa ameshindwa kuomba kutokana na changamoto ya vyeti.

Muda mfupi kabla hajamaliza chuo waliomba wanafunzi wote wapeleke vyeti original baada ya hapo walirudishiwa, but waliokuwa wanadaiwa ada pamoja na yeye hawajapewa vyeti vyao mpaka leo.

Najua humu kuna watu wajuzi zaidi kwenye kila jambo so nahitaji uzoefu na msaada ni namna gani anaweza kufanikiwa kuomba ajira serikalini maana licha ya kufaulu vizuri kule chuoni kuna deni la zaidi ya milioni moja na nusu na hali ya uchumi kwa sasa bado hairuhusu kulipa lile deni.

Naomba msaada wenu wadau wa namna gani atafanikiwa katika hili?
 
Changamoto iliyopo tangu ajira zimetangazwa mara ya kwanza na hata sasa ameshindwa kuomba kutokana na changamoto ya vyeti
Muda mfupi kabla hajamaliza chuo waliomba wanafunzi wote wapeleke vyeti original baada ya hapo walirudishiwa,but waliokuwa wanadaiwa ada pamoja na yeye hawajapewa vyeti vyao mpaka leo.
Yaani kabla ya kumaliza chuo walishapewa vyeti?
 
Ongea na Mtu wa Kati anayefanya Kazi Sehemu panapo-hifadhiwa vyeti then mpoze akuchomolee cheti chako ili ufanye application hii mbinu inahitaji kuongea na mtu ambaye mara nyingi anafahamu vyeti vinapotunzwa mpe 300k

Hii njia ni illigal so ni umakini ndo unahitajika.
 
Kaongee na uongozi alipe hata nusu na kupata cheti chake. Au akishinda amtafite secretary amfanyie maujanja. Usikute wameshasahau Kama wanawadai watu kwahiyo hata nusu watashukuru
 
Yaani kabla ya kumaliza chuo walishapewa vyeti?
Hapana namaanisha waliambiwa wapeleke vyeti original vya form four lakini hawakurudishiwa tena mpaka mtu amalize kulipa madeni yote ndio anapewa cheti chake cha form four pamoja na cha chuo
 
Back
Top Bottom