Nifanyeje kuepuka huu weupe wa Air condition (AC)

Nifanyeje kuepuka huu weupe wa Air condition (AC)

Mgodo visa

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2016
Posts
3,590
Reaction score
3,632
Habarini za mchana wana JF, wajuzi katika jukwaa la JF Doctor.

Nimekuwa muathirika na huu mfumo wa hewa ya kutengenezwa....

Nilikuwa na weusi ambao kwa namna moja nilijivunia pamoja na kuwavutia warembo.

Nowdays nimekuwa na weupe kama mtoto wa Mama au wale wavulana wanaohisiwa ama kutambulika kama watoto si riziki.

Air condition imenifanya nimekuwa mlaini (soft) kama mtu ambaye sikupitia mafunzo ya Jeshi...!!

Naombeni ushauri, nifanyeje kuiepuka hali ama mabadiriko haya..
 
Toa hiyo air condition chumban mpaka ofisini na ukiwa ndani ya gari usitumie kiyoyozi kabisa
Uwezekano wa kuitoa haupo...!!
Niko katika ofisi (kampuni) ya watu, ni mara nyingi tu, nimejiingiza Katika mzozo na Staff wenzangu kwa kuizima mara kwa mara.

Nimeweza kuidhibiti hii ya kwenye gari, kwa kuvuta hewa nikiwa nimefungua Vioo, shida inabaki mahala hapa ninapo patia Riziki yangu.

Natumia Mafuta ya kawaida tu kupaka mwilini (ya Nazi) pia vyakula nakula, kama watanzania wengine tu kwa 100%

Nimechoka na nahisi kuikimbia hali/kazi hii, mana nahisi kupoteza uanaume wangu..
 
Ngoja sasa na Mimi nianze kuifungia kaz AC, naamini ndani ya mwez nitakua mweupo, ole wako kama umedanganya yatakutokea Yale ya watu wasiojulilana
 
Kiongozgi pesa nayo inatakatisha labda umelizika, maana weusi mwingine unasababishwa na stress
 
Back
Top Bottom