Nifanyeje kuku wangu waendelee kutaga?

Nifanyeje kuku wangu waendelee kutaga?

laticka

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2011
Posts
344
Reaction score
130
Wadau salam,
Ninafuga kuku wa kienyeji, nimewalisha vizuri na wametaga kwa muda sasa. Kila walipotaga niliondoa mayai. Nilisafiri wakawa wanaokota mayai vijana, niliporudi nilikuta kuku 49 wanalalia mayai hewa na hawataki KUTAGA tena. Mi natamani waendelee kutaga, nifanyeje?
 
Wafungie kwenye chumba special yaani jela siku mbili bila kuwapa chakula chochote then waachie na uwape chakula kizuri hawataweza kulalia tena maana huwa wanapoteza memory
 
wawekee primix kwenye chakula,

hii kitu unayoiita primix nilikuta ganda la konokono ambalo halijasagwa, sijui waliweka la nini!

Ningependa kujua madini/chakula gani wanaweka humo kusaidia kurudisha kutaga, maana mwingine aliniambia nitumie GLP.
 
unafuga au unatania?. waache waatamie kama unataka mayai mengi ungerifuga wa kisasa. kumbuka hao ni kuku wa asili razima watage na kuatamia, usiwachoshe
 
kiasilia kuku wa kienyeji akitaga baada ya muda fulani lazima alalie, tena kunawengine akitaka kisha ukaondoa mayai sehemu alipotagia, hata taga tena ndo maana huwa wanasema akitaga matatu ondoa acha moja, akija anaona hayatoshi kulalia anaongeza kisha unaondoa unaendelea hivyo hivyo.

ukitaka kuku kwa ajili ya mayai mengi tafuta kuku chotara, mchanganyiko wa kienyeji na kisasa, mimi nina mitetea kumi napata mayai kumi kila siku, tena mayai makubwa sana.
 
Back
Top Bottom