Nifanyeje kumwepusha mwanangu kupatiwa Chanjo?

sinajinasasa

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2013
Posts
2,988
Reaction score
4,152
Habari JF!

Najua humu ndani kuna watu wana akili sana, hivyo kwa michango yenu najua nitatatuliwa huu mtego nilionao.
Mke wangu amejifungua salama mtoto wa kike hivi majuzi, mtoto ni mzuri na afya yake pia maana mtoto amezaliwa na kg 4.9, wote na mama yake wako vizuri.

Tatizo langu ni hizi kinga wanazopewa watoto, huwa sizipendi kwani naona zinaleta shida kwa mtoto. Bahati nzuri muda aliozaliwa ilikuwa ni usiku weekend, watoa chanjo hawakuwepo, wazalishaji walisema asitoke hospitali hadi apate chanjo ya kifua kikuu BCG, bahati nzuri akatoka bila kupewa hiyo chanjo.

Najiuliza hiyo chanjo ina msaada gani? Kwa vile mtoto ataishi kwenye mazingira salama, wazazi tuna kinga ya kutosha kupambana na TB, kwani mtoto yeye si anakinga yake anaponyonya, tena itaendelea kuongezeka?

Wasiwasi wangu ni madhara atakayopata mtoto baada ya hayo makinga, maana najua mtoto lazima apate homa joto kupanda, kukosa hamu ya kula.
Nataka nisimpe kabisa kinga mtoto, bali nimlee vizuri bila kum expose kwenye risk.
Tatizo mama yake pia hana misimamo kama yangu anaogopwa kusimangwa na watu wa clinic za watoto.

Nauliza, kwani sheria za nchi zinalazimisha kila mtoto anayezaliwa apate kinga hizo. Je nifanyeje ili kuepusha asipate hizo kinga?
 
Mpeleke akapate chanjo...nitarudi baadae mkuu.
 
Kwanza nianze kwa kukwambia kinga ya Mtoto ni muhimu wakati mwingine baada ya kuzalia (inborn artificial immunity) hii humsaidia Mtoto kupambana na magonjwa pale kabr hajaanza kujitengenezea kinga,
Ko kwa sababu ya mazingira, nimuhimu apate kinga,
Sasa hapa inatehemeana na attention ya family [emoji128],
 
mkuu mpe chanjo mtoto.. huyo mtoto atakuwa anaenda clinic, kanisani, na maeneo ya mikusnyiko je hapo unamkingaje na kifua kikuu? pia kinga ya mtoto ipo chini kwa wakati huo so usizembee utampoteza dogo huyo
 
Elimu Elimu Elimu

Kuna chanjo za kuupuzia hasa zile za Ukubwani (huko mashuleni) ila sio hizi za watoto chini ya miaka 5. Maana Surua yake, Pepopunda yake, Tetekuwanga yake, degedege lake.

Peleka mtoto akapate chanjo, Pia siku hizi mtoto akiugua wanaangalia sana maendeleo ya kwenye kadi, sasa kimbembe wakute kwenye kadi upande wa chanjo hakupata na ilitakiwa apate. Omba Mungu uwe na hela ila usiwe kama mimi.
 
Habari JF!

Najua humu ndani kuna watu wana akili sana, hivyo kwa michango yenu najua nitatatuliwa huu mtego nilionao.
Mke wangu amejifungua salama mtoto wa kike hivi majuzi, mtoto ni mzuri na afya yake pia maana mtoto amezaliwa na kg 4.9, wote na mama yake wako vizuri.

Tatizo langu ni hizi kinga wanazopewa watoto, huwa sizipendi kwani naona zinaleta shida kwa mtoto. Bahati nzuri muda aliozaliwa ilikuwa ni usiku weekend, watoa chanjo hawakuwepo, wazalishaji walisema asitoke hospitali hadi apate chanjo ya kifua kikuu BCG, bahati nzuri akatoka bila kupewa hiyo chanjo.

Najiuliza hiyo chanjo ina msaada gani? Kwa vile mtoto ataishi kwenye mazingira salama, wazazi tuna kinga ya kutosha kupambana na TB, kwani mtoto yeye si anakinga yake anaponyonya, tena itaendelea kuongezeka?

Wasiwasi wangu ni madhara atakayopata mtoto baada ya hayo makinga, maana najua mtoto lazima apate homa joto kupanda, kukosa hamu ya kula.
Nataka nisimpe kabisa kinga mtoto, bali nimlee vizuri bila kum expose kwenye risk.
Tatizo mama yake pia hana misimamo kama yangu anaogopwa kusimangwa na watu wa clinic za watoto.

Nauliza, kwani sheria za nchi zinalazimisha kila mtoto anayezaliwa apate kinga hizo. Je nifanyeje ili kuepusha asipate hizo kinga?
Ushauri wangu,
Mpeleke mtoto apate chanjo, kuna magonjwa ambayo yanaweza kumshabulia mtoto akiwa ndogo hata baadae atakapo kuwa mkubwa, na yanaweza kusababisha kifo au ulemavu.
Kwa mfano: Ugonjwa wa kuharisha, kifua kikuu, surua, polio. Ni magonjwa hatari sana kaka.
 
"bahati nzuri akatoka bila kupewa iyo chanjo"
.
.
pumbafu kabisa we baba hujui hilo toto lako litakuja kuwa abnormal sijui utamlaumu nani
unataka kumuua mtoto bila hatia ndugu yangu?

Nadhani hakukuwa na haja ya kumnanga mtoto kwa ujinga wa baba yake. Hakuna toto bali ni mtoto.
 
Kaka we umesoma kweli? Ivi kweli hujui umuhimu wa chanjo
 
Sheria ya Afya ya Jamii inamtaka mzazi/mlezi kuhakikisha kuwa mtoto yeyote anayezaliwa anapata chanjo husika ndani ya mwaka mmoja tangu kuzaliwa.

Aidha unaposema ninyi mna kinga na mtamlinda asiambukizwe na magonja kumbuka kuwa hata ninyi mmepata hiyo kinga kwakuwa mlichanjwa, sasa ninyi hamtaki achanjwe hiyo kinga ataipata wapi?

Na km kwa sasa unaogopa hayo unayoita madhara ya chanjo, je unafikiri madhara hayo (ya muda) ni aghali zaidi ya madhara atakayoyapata asipochanjwa kabisa?
 
Chanjo ya BCG
BCG, au Bacille Calmette-Guerin, ni chanjo yenye (contains) sampuli ya bakteria hai, waliopozwa nguvu wa Mycobacterium bovis wajulikanao kama Bacillus Calmette-Guerin ili kutumia vijichembe vya bakteria hao (antigens) kuuamsha mwili wa mtoto utengeneze kinga mtambuko dhidi ya bakteria hatari zaidi wa TB (Mycobacterium tuberculosis), ukoma (Mycobacterium leprae) na ugonjwa wa miliary.

Kwa kesi ya TB ikumbukwe pia kuwa kinga hiyo ni madhubuti tu kwa TB ya uti wa mgongo, na si TB ya mapafu. Ufanisi wake ni mdogo sana ktk kumkinga mtoto dhidi TB ya mapafu na tafiti zaonesha ufanisi wa kinga hiyo ktk kumkinga mtu/mtoto dhidi ya TB ya mapafu unatofautiana kulingana na geographical location ya nchi husika. Ufanisi huo unapungua zaidi kadiri tunavyokaribia mstari wa Ikweta toka North/South poles.

Chanjo ya BCG hutolewa kwa watoto ambao hawana TB lakini wanaishi ktk mazingira yenye ugonjwa wa TB kwa kiasi kikubwa na hawatenganishwi na watu wazima ambao:
• wanaumwa TB na hawajatibiwa kabisa au wamepata tiba isiyo timilifu, au
• wana TB inayosababishwa na vijidudu sugu visivyosikia dawa za kawaida za TB kama isoniazid na rifampin.
Side effects
  • Malengelenge
Inaweza tokea malengelenge sehemu ilipochomwa sindano mara baada ya kinga hiyo. Hii ni kawaida na usipatwe na wasiwasi ikitokea.
  • Kovu la sindano ya BCG
Wiki mbili hadi sita baada ya sindano, kovu dogo linaweza kuonekana katika sehemu ilipodungwa sindano.
  • Reaction ya Ngozi
Pia inaweza tokea skin reaction lakini hupona baada ya wiki chache.
  • Madhara makubwa (Allergy) kwa chanjo ya BCG

Madhara makubwa kwa chanjo ya BCG ni nadra sana. Hutokea kwa mtu mmoja katika watu milioni waliopata chanjo hiyo na ikitokea hivyo muone daktari.
 
Acha kufanya mchezo na afya ya mwanao. Mpeleke mwanao akapatiwe kinga zote ambazo anastahili kuzipata. Acha mawazo yasiyo na msingi Mkuu.

Habari JF!

Najua humu ndani kuna watu wana akili sana, hivyo kwa michango yenu najua nitatatuliwa huu mtego nilionao.
Mke wangu amejifungua salama mtoto wa kike hivi majuzi, mtoto ni mzuri na afya yake pia maana mtoto amezaliwa na kg 4.9, wote na mama yake wako vizuri.

Tatizo langu ni hizi kinga wanazopewa watoto, huwa sizipendi kwani naona zinaleta shida kwa mtoto. Bahati nzuri muda aliozaliwa ilikuwa ni usiku weekend, watoa chanjo hawakuwepo, wazalishaji walisema asitoke hospitali hadi apate chanjo ya kifua kikuu BCG, bahati nzuri akatoka bila kupewa hiyo chanjo.

Najiuliza hiyo chanjo ina msaada gani? Kwa vile mtoto ataishi kwenye mazingira salama, wazazi tuna kinga ya kutosha kupambana na TB, kwani mtoto yeye si anakinga yake anaponyonya, tena itaendelea kuongezeka?

Wasiwasi wangu ni madhara atakayopata mtoto baada ya hayo makinga, maana najua mtoto lazima apate homa joto kupanda, kukosa hamu ya kula.
Nataka nisimpe kabisa kinga mtoto, bali nimlee vizuri bila kum expose kwenye risk.
Tatizo mama yake pia hana misimamo kama yangu anaogopwa kusimangwa na watu wa clinic za watoto.

Nauliza, kwani sheria za nchi zinalazimisha kila mtoto anayezaliwa apate kinga hizo. Je nifanyeje ili kuepusha asipate hizo kinga?
 
Yeye (mtoto) pia anaweza kuwa chanzo cha kuleta maambukizo kwa wenzake kama hatapata kinga zote husika.

Back
Top Bottom