Nifanyeje mtu wa pembeni asione ninachofanya kwenye PC yangu?

Mlatino Zeshalo

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2014
Posts
2,130
Reaction score
3,599
Habari wakuu,

Nipo ofisini katika kampuni fulani. Ninapitia wakati mgumu sana kwani meza yangu ipo angle mbaya sana. Boss wangu ambaye ni CEO wa kampuni anaona kila kitu nachofanya kwenye PC yangu.

Hii PC inaonesha clear sana kiasi kwamba hata mtu aliye umbali flani ananizoom vizuri. Nimepunguza mwanga mpaka mwisho lakini bado inaonekana vizuri tu

Mwenye kuelewa program gani naweza kuinstall ili mtu wa pembeni au aliye umbali wa mita kuanzia mbili asione nachofanya anisaidie

Natanguliza shukrani
 
Weka tinted protector
 
Kuna zile protector za simu, mtu wa pembeni haoni.
Tafuta kama hizo kwa Pc ndo uangalie hayo ma movie yako kwa raha
 
Bila shaka ww sectary wa boss,mwambie boss hupendi hiyo tabia yake ya kuchungulia
 
Mbona tayari nimeshakuona Mkuu?
 

Daaah tumetoka mbali sana pale ilipokuwa San siro walikuwa wanauza PC used ,nilinunua pentium III ,RAM 128MB ,HD 20GB ,Monitor Chogo 14".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…