Natumaini rafiki yko alipitia hatua zote ikiwemo baraza la usuluhishi na upatanishi CMA,
Kimsingi unapaswa kuhakikisha kuwa hakuna rufaa iliyokatwa dhidi yake...
Baada ya hilo utahitajika kufanya application (Execution order) kuomba mahakama itoe agizo la ulipwaji ktk hiyo mahakama husika yani kuiomba mahakama itoe amri ya kufanyiwa malipo.
Kwenye hiyo execution mtaandika majina, siku ya hukumu, kiasi kilichoidhinishwa, nk ....inataratibu zake maalum za uandishi, ni vizuri ukapata mwanasheria...
Kisha mtaipeleka mahakamani na huko mtapewa certificate ya malipo yenu ikiainisha malipo na namna ya ulipwaji....kumbuka hiyo certificate siyo malipo