Nifanyeje taasisi/serikali inilipe?

cheguevara

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2012
Posts
1,348
Reaction score
652
Habari wadau,kuna rafiki yangu alifukuzwa kazi ktk taasisi moja ya serikali kwa hila tu za boss wake na baadae akaenda mahakama ya kazi na kuonekana kuwa ameonewa hivyo alipwe stahili zake lakini taasisi hiyo haijafanya hivyo je afanyeje kupata haki yake?
 
Natumaini rafiki yko alipitia hatua zote ikiwemo baraza la usuluhishi na upatanishi CMA,
Kimsingi unapaswa kuhakikisha kuwa hakuna rufaa iliyokatwa dhidi yake...
Baada ya hilo utahitajika kufanya application (Execution order) kuomba mahakama itoe agizo la ulipwaji ktk hiyo mahakama husika yani kuiomba mahakama itoe amri ya kufanyiwa malipo.

Kwenye hiyo execution mtaandika majina, siku ya hukumu, kiasi kilichoidhinishwa, nk ....inataratibu zake maalum za uandishi, ni vizuri ukapata mwanasheria...

Kisha mtaipeleka mahakamani na huko mtapewa certificate ya malipo yenu ikiainisha malipo na namna ya ulipwaji....kumbuka hiyo certificate siyo malipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…