Pole sana na hongera kwa kuumia kuona umuhimu wa kutomkosea mwanamke mwenzio,si wanawake wengi wana roho hii hasa kama walimpenda mtu ila kukawa na vikwazo fulani wakashindwa kuwa pamoja.
Kuhusu huyo mke wa huyo kaka,kwanza muelewe tu,ni haki yake kukasirika na kweli inauma sana na kuleta maswali mengi......kubadili namba,wala kumu ignore kunaweza kusiwe suluhisho na pengine akafikiri vingine na hasira yake ikazidi.....zungumza na huyo dada kwa upole na kwa maneno machache sisitiza huna uhusiano na mumewe tena....usimjibu kwa hasira hata kama amekuudhi sana,baada ya muda atatulia na mwaweza kaa chini mkazungumza......nilishapata adha ya kutukanwa nikizaniwa natoka na mume wa mtu kisa mazoea ya utani utani.....nikakaa chini nikajiweka kwenye nafasi ya yule mwanamke nikamuelewa,nikamtafuta akanitukana wee baadaye nikamuomba mumewe atukutanishe mimi na yeye lunch.....akafanya hivyo,niliongea nae kwa masaa mawili......tangu siku hiyo mimi na yeye tu marafiki sana.....yaani wale wa kusikilizana kwenye mambo magumu sana na kusaidiana na bado tu marafiki na mumewe......
Itachukua muda yeye kukuelewa,ila naamini baada ya muda atakuelewa vizuri tu.....pengine haufahamu ukweli,sisitiza kwa maneno na matendo yako kuwa huna uhusiano na mumewe uliokuwa nao huko nyuma na kwamba una heshimu ndoa yake na Mungu....kama huu ndo ukweli,siku si nyingi utamuona tu kapoa na maisha yanaendelea.....mumewe hakufanya vizuri kwa maoni yangu,yaonekana ni mtu wa mabavu na hili laweza mgharimu sana......
all the best dear.....Mungu akuepushe na mabaya yote manake siku hizi watu wana hasira,akikuhisi tu hashundwi kukufanya baya....mshirikishe pia Mungu,yeye aujua ukweli na ana nguvu ya kutuliza yote haya!