Naomba mnifanyie thathmini ya kazi yangu katika video hapa chini. Ni tangazo fupi la TV. Sijahusika kutengeneza sauti katika tangazo hili, nimehusika katika visual part.
Ningependa tathmini iangalie uhusiano wa matukio na message husika, pia uzuri kwa maana ya beauty ya graphics/animations. Ikiwezekana wachambuzi waniambie uzito (impact) wa tangazo hili (chance ya kuwa ignored na watazamaji) n.k.
NB. Nakaribisha maoni ya aina yoyote toka kwa yeyote, si lazima yawe technical pekee.
huo mlima uko too fake. weka animations mbili tatu za mifano ya hao wajasiria mali. Huyu mtu mwenye suti anyezunguka zunguka hapo anamaanisha chochote?
jamaa anasema the following categories..... halafu kuna break the hizo categories hazijaonyeshwa wala kutajwa isipokuwa kwa ujumla wake. Unless aseme kabisa 24 categories.....
Pia ingependeza kama lingetengenezwa la kiswahili...
Umenichekesha Dr unaposema ningepindisha kidogo mambo ndo nione michango ya mawazo. Actually 90% ya kazi hii si 3D, ni 2D ya Adobe AfterEffects na rest ni 3D kidogo tangazo linapoanza. I'll be posting more of my 3D works in the near future, zitakuwa a bit heavier. Currently nafanyia kazi suala la character animation. Inanichukua muda mrefu kwa kuwa najifunza mwenyewe na nimebanwa na mambo ya hapa na pale ila within a year nadhani nitakuwa nime-master character animation. By the way nafikiria ku-release sinema itakayokuwa supported sana na CGI kati ya December 2012 na June 2013. Animated Film natarajia niitoe June 2014 if God wishes.
huo mlima uko too fake. weka animations mbili tatu za mifano ya hao wajasiria mali. Huyu mtu mwenye suti anyezunguka zunguka hapo anamaanisha chochote?
Thanks for your comments. Ni kweli kuwa ukitazama mlima utagundua kirahisi kuwa mlima unaonekana kuwa too fake, I'll work on that. Kuhusu mtu mwenye suti, waliotaka nitengeneze tangazo walitaka kitu kama hicho kwa maelezo kuwa inawakilisha mtu mwenye vision (tazama maneno yaliyoandikwa karibu yake - From a Vision.. to a dream come true).
jamaa anasema the following categories..... halafu kuna break the hizo categories hazijaonyeshwa wala kutajwa isipokuwa kwa ujumla wake. Unless aseme kabisa 24 categories.....
Pia ingependeza kama lingetengenezwa la kiswahili...
Kulikuwa na ubishi sana hapa wakati wa utengenezaji. Mwanzoni ilkuwa categories ni nne, na nikatengeneza tangazo likaisha, then wakaja na ideas mpya za kuongeza categories. Kasheshe ikawa huwezi kuzionesha categories zote at a time na zisomeke ukitilia maanani pia tangazo nii lazima lisizidi 45 seconds ambazo wadhamini walikuwa tayari kulipia, mwishowe uamuzi ukawa maandishi ya categories yapite chini hadi tangazo linapoisha. Kwenye kazi hizi sometimes huwa kuna tofauti za mawazo na challenges za deadlines. Kuhusu Kiswahili ni kweli unachosema lakini client alikuwa anataka Kiingereza pekee, nadhani aliowatarget si wajasiriamali wasiojua Kiingereza.
Tangazo hili litaanza kurushwa katika TVs hivi karibuni. Thanks again for your comments.