Mfanyabiashara na mwanamitandao maarufu nchini, Jennifer Bilikwija ‘Niffer’, amewasha moto wa mjadala kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuweka wazi mtazamo wake kuhusu ushikaji na wanawake wenzake.
Niffer amebainisha kuwa ingawa anawapenda na kuwaheshimu wanawake, hana mpango wala uwezo wa kujenga urafiki wa karibu mno nao. Through kauli yake iliyoambatana na emoji za kucheka, mrembo huyo alisema:
“Yaani nawapenda wanawake wenzangu ila kuwa na urafiki wa karibu nao siwezi kabisaaaa.”
Kauli hiyo imewaganya mashabiki na wafuatiliaji wake katika makundi mawili; wapo waliomuunga mkono wakidai urafiki wa wanawake mara nyingi una changamoto nyingi, huku wengine wakihisi huenda kauli hiyo imetokana na uzoefu wake wa nyuma au ilikuwa ni ya utani tu.
Urafiki wenu nyie wanawake mara nyingi huwa umejaa drama nyingi sana. Leo mko vizuri, kesho mnasengenyana na kuibiana siri zenu. It's too exhausting, Kwa mtu ambaye biashara zake zinahitaji peace of mind, ni sawa tu kuamua kufanya hivyo.
Yuko sahihi ..
Urafiki baina yenu wanawake mara nyingi hua ni wamashaka. Sababu wengi wenu ndio chimbuko la uongo, husda, wivu, fitina , uchawi na uzandiki