Nifuate malengo yangu au niisikilize jamii ?

ntita

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2013
Posts
513
Reaction score
285
wana jf.
mimi ni mhitimu wa kdt cha 6 pcm. ufaulu wangu ni dv 1 pt 7. malengo yangu ni kusoma physics nikiwa chuo jambo ambalo linanilazimu kuichukua na education kwa bachelor degree ili niingie ktk soko la ajira kabla sijachukua masters na kuendelea. lakini kuna ndg haungi kabisa mkono wazo hili hasa ukizingatia wengi huchukulia anayesoma edu kama aliyefeli. sasa niko njia panda naombeni ushauri wenu. natanguliza shukurani
 
Una kipaji soma kijana uje kukomboa taifa hili tegemezi. Tunataka wataalamu wa kugundua vitendea kazi vya kutuletea maendeleo haraka.
 

hongera kwa kufaulu mdogo wangu ila soma unachokihitaji ndugu wanaweza kukupeleka pabaya wanakushauri kusomea kitu kingine afu ukimaliza kazi hakuna na wenyewe huwaoni
 
Una kipaji soma kijana uje kukomboa taifa hili tegemezi. Tunataka wataalamu wa kugundua vitendea kazi vya kutuletea maendeleo haraka.

ndo niko njia panda sasa kuhusu nini cha kusoma maana malengo yanaonekana kutofautiana na mtazamo wa jamii.
 
kapige hiyo edu kjana; najua baada ya masters utakuwa mhadhii wa chuo achana na hao wanaokudanganya ualim hauna dil
 

Soma unachokipenda maswala ya ajira achana nayo.
 
kwa ushauri wako nisome nini badala yake.

simply, fuata moyo wako piga hata petroleum engeneering ina deal sana hii, mi sikushauri ualimu utakauja juta siku moja.
 
Soma kile kinachokusukuma moyoni ucje ukaja ukajuta mbeleni kwa kile ulicho ambiwa usomee wakat hayakua n malengo yako. Ukifanya kitu unachkipenda lazima utakiheshimu na kukifanya kwa jitihada hekima busara na weledi ili uweze kuktimiza. BA in physics ni big deal sana, Taifa linahtaj waalimu wa masoma ya sayansi waliofaulu kwa kiwango cha juu kama wewe. Huta sumbuliwa swala la ajira tena ukifaulu vizuri kwa chuo kama UDSM unaweza ukabakishwa na kusomeshwa masters bure huku ukilipwa na mshahara.ila usickua mawzo ya watu ndo ukayafanyia kazi bali changanya na ya kwako pia alafu utatka na kitu cha maana sana.
 

nikisema asante watasema nilikuwa na uchaguzi tayari. lakini umeongea kitu cha muhimu sana.
 
kapge ualimu pia uwe mvumilivu maana hata hayati baba wa nchi yetu alipakimbia huko...
 
Kama lengo ni kuingia kwenye soko la ajira nenda kasome civil eng !!!!
 
una maana gani?

Nyepesi tu hv muasisi wa hili taifa alikuwa mwalimu lakini akaona haumfai so akakabidhi chaki kwa wenye nia na hii fani ye akajiendea zake state house...ujue we una bahati ila unataka kuichezea bongo sio kama mtoni wewe huku walimu ndo lower class..,kapge coz ya maana stop thinking of tht shit as it wil waste ur time to take you where you are required to be...
 
kama unataka mafanikio ya mkupuo achana na ualimu lakn kama unataka kwnda mdogomdogo hamna shida kwanza mkopo 100% na ajra zpo,jeeaah...
 
Nakushauri achana na ualimu hiyo ni ajira yenye watumishi wengi sana hivyo nchi yetu imeshindwa kabisa kuwathamini hata wale Wa masomo ya sayansi ambao ni wachache na muhimu.

Kasomee kozi za wachache katika soko la ajila hususani masomo ya engendering kwani physics bado utaisoma tu.

Na hata ukisoma masomo ya engeneering bado unaweza ukawa lecture Wa vyuo vikuu kwa hiyo ndoto yako ya kufundisha inakuwepo kwenye maslahi au unaweza hata kujiajili na bado scholarship utapata za masters kwa masomo ya engineering ili mradi ufaulu vizuri tu.

Lakini si ualimu Wa sekondari au msingi kwa nchi hii acha kabisa, hawathaminiwi, ndugu zetu wako huko wanajuta kufanya wrong selection ya kozi walipo kuwa hatua kama yako,kisa ajila ya uhakika.sasa wanasaidiwa na wadogo zao wenye certificate na diploma za field tofauti.

Tafakari, chuja na wasiliana na halmashauri ya ubongo wako kisha chukua hatua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…