Niger vs Taifa Stars | Tufanyeje kuweza kuwafunga Jumamosi?

Niger vs Taifa Stars | Tufanyeje kuweza kuwafunga Jumamosi?

Moshi25

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2022
Posts
2,555
Reaction score
4,118
Wanabodi.

Mbona naona kama wabongo hatuna kabisa mzuka na hamasa kwa timu yetu ya Taifa? Shida ni nini? hakuna uzi nyingi humu why?

Wangapi tuna mpango wa kuiombea na kuishangilia timu yetu ya Taifa ikiipasua Niger jumamosi hii?

Samatta mechi za kirafiki ameonesha ni mzuri sana kwa assist kuliko kulazimisha kufunga!!

Timu yetu huwa inakata pumzi kuanzia dakika ya 60 hivi tunaanza kushambuliwa mwanzo mwisho, hivi Mwalimu Kim analijua hilo? Amefanya nini kurekebisha? TFF nao wamefanya nini kurekebisha hilo? Media hasa Clouds Fm redio pendwa imefanya nini kurekebisha hilo?

List gani tunapenda kuona ikianza? taja first eleven yako!

Maoni yangu kwa wachezaji wajivunie kuitwa Timu ya Taifa, walipiganie taifa Lao, wajitume uwanjani mechi zote 6, wajiamini na uwezo wanao na tucheze kwa jihadi kila mechi kama fainali tusisubiri ile staili yetu ya kuombea timu flani ifungwe eti ndo tupite.

Hakuna mchezaji wetu kuchekacheka akikosa goli au baada ya mechi kuisha tukiwa tumefungwa, wajue wabongo tunaipenda timu yetu na tabia hiyo inatuchukiza sana

Hakuna kubadilishana jezi zetu na wapinzani.

Hatuhitaji selfie tunataka magoli! Tukifunga goli nne bila itapendeza zaidi!!

Je tufanye nini tuwafunge Niger jumamosi?

Nawasilisha
 
Wanabodi.

Mbona naona kama wabongo hatuna kabisa mzuka na hamasa kwa timu yetu? Shida ni nini? hakuna uzi nyingi humu why?

Wangapi tuna mpango wa kuiombea na kuishangilia timu yetu ya Taifa ikiipasua Niger jumamosi hii?

Samatta mechi za kirafiki ameonesha ni mzuri sana kwa assist kuliko kulazimisha kufunga!!

Timu yetu huwa inakata pumzi kuanzia dakika ya 60 hivi tunaanza kushambuliwa mwanzo mwisho, hivi Mwalimu Kim analijua hilo? Amefanya nini kurekebisha?

List gani tunapenda kuona ikianza? taja first eleven yako!

Maoni yangu kwa wachezaji wajivunie kuitwa Timu ya Taifa, walipiganie taifa Lao, wajitume uwanjani mechi zote 6, wajiamini na uwezo wanao na tucheze kwa jihadi kila mechi kama fainali tusisubiri ile staili yetu ya kuombea timu flani ifungwe eti ndo tupite.

Hakuna mchezaji wetu kuchekacheka akikosa goli au baada ya mechi kuisha tukiwa tumefungwa, wajue wabongo tunaipenda timu yetu na tabia hiyo inatuchukiza sana

Hakuna kubadilishana jezi zetu na wapinzani.

Nawasilisha
vipindi vyooote vya michezo vinamjadili ntibazonkiza, pablo (kocha wa madrid), na morrison
magazeti yanajadili hivyohivyo
radio zinatangaza kamari tuuu
 
wanajadili, mama kuupiga mwingi, kamari kila radio na kila TV, kocha wa simba na wachezaji wa kimataifa, na mbape kuhama. Ndicho ninachokisikia aisee
 
Back
Top Bottom