Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 417
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) limetoa ripoti inayoangazia madhara ya mapigano katika eneo la Kaskazini mwa Nigeria, likikadiria kuwa athari za mgogoro huo ni kubwa mara 10 zaidi ya makadirio ya athari yaliyotolewa awali.
Awali, Shirika hilo lilikadiria kuwa takriban watu 35,000 walifariki dunia kutokana na mapigano hayo, ambapo takwimu hizo ziliangazia wale tu waliofariki katika mapigano. Utafiti mpya umebaini kuwa zaidi ya watoto 324,000, wenye umri chini ya miaka 5 wamefariki katika mapigano yanayoendelea kwa mwaka wa 12 sasa. Katika kila vifo 10, tisa ni vya watoto, huku 170 wakifariki kila siku.
Kukosekana kwa usalama kumesababisha kudorora kwa shuguli za kilimo na biashara, huku sehemu kubwa ya wakazi wa eneo hilo wakitegemea kilimo kama njia kuu ya kiuchumi. Kati ya vifo 350,000 vilivyotokana na mapigano hayo, inakadiriwa vifo 314,000 vimetokana na sababu zisizo za moja kwa moja.
Maeneo yaliyoathirika zaidi na mapigano hayo ni ya majimbo ya Borno, Adamawa na Yobe, kwa mujibu wa ripoti hiyo. Rais wa Nigeria yupo katika shinikizo kubwa kumaliza mgogoro huo.
Chanzo: Al Jazeera.