Nigeria: Klabu ya Plateau yagoma mchezo wake dhidi ya Simba Sc unaweza usiruke 'Live'

lui03152

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2020
Posts
266
Reaction score
377
NIGERIA: Plateau Utd wamekataa kuruhusu mechi kurushwa mubashara. Licha ya juhudi zetu zote tukishirikiana na mshiriki wetu AZAM TV, mwenyeji wetu amekataa kushirikiana kwenye hilo.

Nichukue nafasi hii kuomba radhi kwa wapenzi wetu wote ulimwenguni ambao walitaka kuangalia mechi hii.

Mpaka muda huu, tunapigania hii mechi iweze kuoneshwa mubashara (live).

— Barbara Gonzalez
Mtendaji Mkuu, Simba Sports Club
 
Hivi bado kuna watu wanaishi zama za "giza?"
 
Wanaogopa kuoga magoli,maana hii tinu haijawahi kufanya mazoezi kabisa
 

Pls ....reason behind? what about SuperSport?
 
Mpira wa kiafrica figisu sana.
Ngoja na wao wakija kwetu tuwaoneshe Ngondo.
 
Pls ....reason behind? what about SuperSport?
Mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa kati ya Plateau United dhidi ya Simba ambao utapigwa baadae leo uwanja wa New Jos huko Nigeria, hautaonyeshwa mbashara

Imeelezwa kuwa maafisa wa Plateau United wamegoma mchezo huo kurushwa mbashara licha ya juhudi kufanywa na Ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria kuomba Azam TV wapewe haki ya kuonyesha mchezo huo

Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Dk Benson Bana amesema Plateau United wamegoma mchezo huo kurushwa mbashara hivyo amewataka Watanzania kuiombea Simba iweze kufanya vizuri kwenye mchezo huo

Uongozi wa klabu ya Simba umethibitisha kuwa mchezo huo hautakuwa mbashara kwenye kituo chochote cha televisheni

"Kwa masikitiko tunawajulisha Wanasimba na Watanzania wote kwamba mchezo wetu wa kesho dhidi ya Plateau United hautaonyeshwa mbashara baada ya wenyeji wetu Plateau kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya mchezo huo"

Hakuna chombo chochoto kitakachoonyesha mkuu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…