beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Polisi nchini Nigeria imewaokoa watu 259 kutoka katika kituo kisichokubalika kisheria kilichopo ndani ya msikiti katika mji wa Ibadan, uliopo katika jimbo la kusini magharibi mwa nchi hiyo la Oyo, vimeripoti vyombo vya habari nchini humo.
Wengi miongoni mwa waliookolewa katika uvamizi wa polisi walikuwa wamefungwa kwa minyororo katika eneo la msikiti, amesema msemaji wa Polisi Gbenga Fadeyi.
Katika kipindi cha uliopita, zaidi ya watu 1,000 wameokolewa kutoka kwenye vituo vya kidini ambako mara kwa mara watu wamekuwa wakishikiliwa katika hali mbaya.
Wazazi wamekuwa wakiwatuma watoto wanaowasumbua kitabia na vijana wanaoaminiwa kuwa na uraibu wa madawa ya kulevya au wale waliopatikana na makosa madogo katika vituo vya Quran vya kurekebisha tabia.
Lakini maafisa wamevifananisha vituo hivyo na vituo vya ukatili ambapo watu wanafungwa minyororo, kufungwa pamoja na kufanyiwa dhuluma.
Waliotekwa waliachiliwa Jumatatu jioni baada ya polisi kupewa taarifa na kijana mwenye umri wa maika 17 ambaye alikuwa ametoroka kutoka katika mahabusu nyingine katika eneo hilo.
Mmiliki wa mahabusu hiyo na watu wengine wanane wamekamatwa, limeripoti gazeti la Punch nchini humo.
Kamishna wa Polisi wa jimbo hilo Bwana Shina Olukolu alinukuliwa akisema kwamba baadhi ya waathriwa wa utekaji huo wamesema wamekuwa wakishikiliwa kwa miaka kadhaa.
Hali katika msikiti huo ilikuwa ni mbaya kwa binadamu kuishi na baadhi ya vifo vya waathirika vilivyotokea havikuripotiwa, alinukuliwa akisema.
Huu ni mojawapo ya uvamizi wa wa hivi karibuni wa vituo vinavyoitwa ''vituo vya kiurekebisha tabia'' nchini Nigeria ambamo watu wanashikiliwa katika hali mbaya mkiwemo kufungwa na minyororo.
Wengi husajiliwa kwenye taasisi hizo na ndugu zao ili kupata usaidizi wa kiroho na kurekebisha tabia kwa wanaotumia madawa ya kulevya.