MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Nigeria ambayo ilikua kwenye miongoni mwa mataifa machache yanayonunia muungano wa Afrkia wenye dhamira ya kufunguliana kibiashara, imekubali itatia saini baada ya kuona mwanga. Hivyo soko la watu zaidi ya bilioni moja linazidi kutanua na kama wasemavyo wengi, yajayo yanafurahisha.
Wakati huo huo Kiswahili chapokelewa kama lugha rasmi ya Afrika, hivyo kwa kufunguliana kibiashara Afrika yote na kufanya Kiswahili lugha yetu, tunakwenda kwa kasi kwenye kuunganisha bara hili. Rais Uhuru anatarajiwa kuhudhuria kikao cha huu muungano mpya wa Afrika utakaofanyika Niamey, NIger. Jitihada zake rais Uhuru ni muhimu sana maana yeye amehusika pakubwa kwenye kuhamasisha muungano kupokea Kiswahili. Ikizingatiwa pia Wakenya wanakwenda Afrika Kusini kufundisha Kiswahili.
Ikumbukwe pia Kenya inashughulika kuhakikisha makao makuu ya huu muungano yatakua Nairobi, hivyo kwa kurasimisha Kiswahili na kwamba Kiswahili ni lugha yetu ya taifa, ina maana Kenya ndio itakua kitovu cha huu muungano.
Wanaoendelea kununa waendelee, labda ipo siku watajishtukia, au waamshwe kwa vibao, japo pia nahisi kununa kwao na usingizi wao ni mtaji wetu
www.businessdailyafrica.com
edition.cnn.com

AU backs Kiswahili as continental language
AU has joined the campaigns to elevate Kiswahili as one of its common languages.
Nigeria will join Africa's vast free trade area
Nigeria has signed the Africa Continental Free Trade Agreement (AfCFTA) which aims to increase trade between African countries.