Nigeria yaadhimisha miaka 57 ya uhuru

Nigeria yaadhimisha miaka 57 ya uhuru

Arnoldius

Member
Joined
Oct 1, 2017
Posts
25
Reaction score
4


na Sabina Chrispine Nabigambo

Nchi ya Nigeria inaadhimisha miaka ya 57 ya uhuru wake,tangu kumalizika kwa utawala wa kikoloni mwaka 1960

Akihutubia taifa hilo hapo Jana Rais Mohammadu Buhari amewataka wanijeria kukumbuka safari ndefu waliyopita hadi kufikia utawala wa kidemokrasia mwaka 2015 na kudumisha umoja wao.

Aidha ofisi ya makamu wa rais Yemi Osinbajo imeorodhesha mafanikio yaliyopigwa na serikali inayoongozwa na rais Buhari tangu aingie madarakani mwaka 2015.

Miongoni mwa mafanikio yanayotajwa ni pamoja na suala la usalama hasa hatua ya kuachiwa kwa wsichana 106 wa shule ya Chibok sambamba na watu 16 000 waliokuwa wametekwa na kundi la Boko Haram

Hata hivyo nchi hiyo bado inakabiliwa na changamoto nyingi za kiusalama na kiuchumi kufuatia uasi unaofanywa na kundi la Boko Haram Kaskazini mwa nchini hiyo.
 
Back
Top Bottom