Night shifts ...changamoto zake ni zipi??!!

Dark City

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2008
Posts
16,253
Reaction score
11,626
Samahani wadau wa jukwaa letu tukufu la MMU,

Kwanza kabisa, naamini mko wazim na mnadunda...Mie pia ni mzima na nimewa-miss kikweli kweli!!

Leo nimejikuta napatwa na mawazo ya ajabu ajabu kuhusu hili jambo ambalo katika makuzi yetu hatukukutana nalo. Enzi zetu mama alikuwa mtu wa shamba na baba anafanya kazi kidogo shamba na kutumia muda wake mwingi kuzunguka mitaa kama jogoo!!

Siku hizi, hiki kizazi kimejikuta kikikabiliwa na changamoto za kimaisha. Ni jambo la kawaida kukuta wanandoa wote wanafanya kazi na mmoja wao au wote wanalazimka kuwa na zamu za usiku.

Kwa wale wenye kazi za namna hiyo au wanafahamu washikaji/jamaa wenye kazi kama hizo, wanaweza kutupatia uzoefu wao kuhusu changamoto za kazi za namna hii especially katika sekta ya MMU??

Wenu awapendaye,

Babu DC!!
 
Ni rahisi kupata mawazo ya usaliti na pengine kumsaliti mpenzi wako kabisa.
 
...mstaafu vipi? kwema...?

...haya bana, madhali umeyataka ya uvunguni ngoja nikupe akiba yangu ya maneno...
kaka, kwenye mapenzi hakuna kazi mbaya...kazi ni kazi almuradi mama watoto anasaidia
kupunguza makali ya maisha...hiyo kazi iwe ni ya mchana au usiku sawa tu...

...la pili, ikiwa ni mtu mwenye wivu sana, basi ombea mkeo afanyae kazi ya kutangaza Tv, au
radioni...maana kwenye luninga si utakuwa unamuona bana,....na radioni unamsikia...lakini jua
pakiwekwa tangazo la biashara au muziki...hizo dakika tano zinatosha kabisa watu 'kuchimba dawa'...

...la msingi kwenye sekta hii ya 'hamadi kibindoni' ni kuaminiana tu na kumuachia mungu afanye maajabu
yake, ..."ukimchungua kuku hutamla!"
 
mtu kama kiwembe ni kiwembe tu hata kama kazi yake ni mchana tu..miye naingia night kama kawaida na bado sijashawishika kumsaliti bby wangu.ila yeye uaminifu zero kabisa,yaani kila mara lazima apige simu hewani.ole wangu niingie operation usiku bila hata kumtext ntakiona cha mtema kuni
 
Kuna jirani yangu mmoja kipindi fulani alikuwa anafanya kazi ya shift na mkewe pia. Alinambia ilifika kipindi wiki nzima hajaonana na mkewe. Ili kujiaminisha kama mkewe anarudi akiondoka anavuruga shuka kitandani. Akikuta kitanda kimetandikwa anaamini mke wake alirudi nyumbani. Alimshawishi mke wake aache kazi bila mafanikio. Mpaka alipoamua mwenyewe kumwaga manyanga na kuwa mjasiriamali.

Mke wake akaendelea kuwa "nyumba ndogo" ya daktari mpaka ndoa ilipovunjika.

Hivi sasa kaamua kabisa kuwa mke wa daktari yule.

Chezeya kazi ya shifti? Full vishawishi!
 
madhara ya kuoa nesi:kila mtoto atakayezaliwa utaambiwa kafanana na marehemu babu yake mzaa mama ambaye hujawahi kumtia machoni.
 
...mstaafu vipi? kwema...?

...haya bana, madhali umeyataka ya uvunguni ngoja nikupe akiba yangu ya maneno...
kaka, kwenye mapenzi hakuna kazi mbaya...kazi ni kazi almuradi mama watoto anasaidia
kupunguza makali ya maisha...hiyo kazi iwe ni ya mchana au usiku sawa tu...

...la pili, ikiwa ni mtu mwenye wivu sana, basi ombea mkeo afanyae kazi ya kutangaza Tv, au
radioni...maana kwenye luninga si utakuwa unamuona bana,....na radioni unamsikia...lakini jua
pakiwekwa tangazo la biashara au muziki...hizo dakika tano zinatosha kabisa watu 'kuchimba dawa'...

...la msingi kwenye sekta hii ya 'hamadi kibindoni' ni kuaminiana tu na kumuachia mungu afanye maajabu
yake, ..."ukimchungua kuku hutamla!"
Khaaa.....................!😛eep:

"Kibelaaaaa..." ...2012 dunia ni yako...:nimekataa:😛ray::rant:...chaguo ni lako.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
...mstaafu vipi? kwema...?

...haya bana, madhali umeyataka ya uvunguni ngoja nikupe akiba yangu ya maneno...
kaka, kwenye mapenzi hakuna kazi mbaya...kazi ni kazi almuradi mama watoto anasaidia
kupunguza makali ya maisha...hiyo kazi iwe ni ya mchana au usiku sawa tu...

...la pili, ikiwa ni mtu mwenye wivu sana, basi ombea mkeo afanyae kazi ya kutangaza Tv, au
radioni...maana kwenye luninga si utakuwa unamuona bana,....na radioni unamsikia...lakini jua
pakiwekwa tangazo la biashara au muziki...hizo dakika tano zinatosha kabisa watu 'kuchimba dawa'...

...la msingi kwenye sekta hii ya 'hamadi kibindoni' ni kuaminiana tu na kumuachia mungu afanye maajabu
yake, ..."ukimchungua kuku hutamla!"

Ahsante sana kaka,

Kweli sikutaka kujua kama kazi yenye shift ni nzuri au mbaya...ila kama vile kazi nyingine zilivyo na changamoto zake, nilitaka kujua spefically changamoto za kuwa tu unakuwepo kibaruani usiku!!!

Si unajua Mungu aliweka usiku tupumzike na kufanya majukumu machache tu, but yet, muhimu sana!!!???

Babu DC!!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Ni rahisi kupata mawazo ya usaliti na pengine kumsaliti mpenzi wako kabisa.

Dadavua kidoho ili tupate uhondo Hus,

Inaonekana uko fully informed au vipi??

Babu DC!!
 
mtu kama kiwembe ni kiwembe tu hata kama kazi yake ni mchana tu..miye naingia night kama kawaida na bado sijashawishika kumsaliti bby wangu.ila yeye uaminifu zero kabisa,yaani kila mara lazima apige simu hewani.ole wangu niingie operation usiku bila hata kumtext ntakiona cha mtema kuni

Suala si kumsaliti au la?

Ni je unakumbana na changamoto gani? Mfano hapo blue...ungekuwa hauko kwenye night shift hali ingekuwa hivyo??

Babu DC!!
 
Changamoto na vishawishi ni nyingi sana kwa watu wasio waaminifu ktk mahusiano. Wako wanaotumia opportunity hizo kutembea na wafanyakazi wenzao, wapo wanatumia visingizio vya night shifts kwenda kwa nyumba ndogo, wengine kwenda kwenye starehe za ajabu ajabu nk. Cha msingi mi nitasisitiza ni uaminifu ndani ya mahusiano au ndoa. Hapo hizi changamoto haziwezi kuwa kikwazo ktk mahusiano
 
Ni kweli kaka,

Kuna story nilipewa kuwa dada mmoja nurse aliaga kwenda kazini. Huko nyuma mtoto kazidiwa na kupelekwa hospitali. Mama alitafutwa lakini hakupatika hapo kazini. Kumbe hakuwa kazini wala nini...alienda kujirusha...

Kilichofuata ni hadithi ndefu tu...but in short, ndoa iliisha siku hiyo!!

Babu DC!!
 
Ukiwa na mwamke/mwanaume anaingia shift basi sehemu ya wivu iondoe kabisa ndani ya moyo wako.
 
raha ya ndoa ni usiku bwana
i cant imagine kama nitapata mume ambae hayupo rechabo usiku
soo sad
 
Back
Top Bottom