BADILI TABIA
JF-Expert Member
- Jun 13, 2011
- 32,767
- 23,198
Unataka kusema manesi sio waaminifu..?
....ok, ok...
Ndoa ni ndoa, haijalishi ni mchana au usiku, hata tendo la ndoa halihusu muda,
kinyume na wanadamu na hulka zao...imefikia kuhusisha tendo la ndoa na chumba, giza pamoja
Na siku za baridi/mvua....
Kazi za shifti haziepukiki...mfano, nurse, doctors, police +security jobs, zima moto, newsroom, etc
vile vile marubani, madereva, na hata Ma DJ na wanamuziki....'sic'
maisha ni makubaliano tu, iwe usiku au mchana...muhimu kuheshimiana, na maelewano.
Dadavua kidoho ili tupate uhondo Hus,
Inaonekana uko fully informed au vipi??
Babu DC!!
kuna mkaka rafiki yangu ana mke anafanya kazi 9t shift. Ngoja nimuulize changamoto anazokutana nazo ila mpaka sasa nimeshanote kuwa huwa anaboreka sana nyakati za usiku na hafurahii.
Babu DC shkamoo.
Babu ni changamoto tu za maisha .
Hichi kizazi chetu cha Dotcom bila fedha
Hatuwezi ishi tofauti kidogo na 47 I guess kipindi hicho bila shamba na mifugo maisha ni utata. Miaka hiyo jembe miaka hii mtumikie mkoloni
Anyhow sababu ya hizi kasi za maisha ya miaka hii lazima tukubali ku sacrifice kitu fulani na ku change time table kwenye vitu fulani fulani ...
Tumezoea. Mfano mzuri tu huu hapa partner anafanya kazi ni Dr. Kwenye emergency Department. (ED) yuko night shift. Mdada ndo anae endesha business zenu zote halafu juu ya hapo mna mtoto ...
Ukiangalia week nzima ni full on. Lakini ile siku ambayo mko off.ndo mambo yote yanafanyika hata na hivyo ni muhimu sana kutafuta masaa matatu au manne kwa siku ajili ya familia ... hizo holidays at least mara mbili kwa mwaka na familia mnaenda mahali kwa wiki 3-4 hivi... maisha ni rush hour siku hizi babu ...
Msalimu bibi ...
...mstaafu vipi? kwema...?
...haya bana, madhali umeyataka ya uvunguni ngoja nikupe akiba yangu ya maneno...
kaka, kwenye mapenzi hakuna kazi mbaya...kazi ni kazi almuradi mama watoto anasaidia
kupunguza makali ya maisha...hiyo kazi iwe ni ya mchana au usiku sawa tu...
...la pili, ikiwa ni mtu mwenye wivu sana, basi ombea mkeo afanyae kazi ya kutangaza Tv, au
radioni...maana kwenye luninga si utakuwa unamuona bana,....na radioni unamsikia...lakini jua
pakiwekwa tangazo la biashara au muziki...hizo dakika tano zinatosha kabisa watu 'kuchimba dawa'...
...la msingi kwenye sekta hii ya 'hamadi kibindoni' ni kuaminiana tu na kumuachia mungu afanye maajabu
yake, ..."ukimchungua kuku hutamla!"
mtu kama kiwembe ni kiwembe tu hata kama kazi yake ni mchana tu..miye naingia night kama kawaida na bado sijashawishika kumsaliti bby wangu.ila yeye uaminifu zero kabisa,yaani kila mara lazima apige simu hewani.ole wangu niingie operation usiku bila hata kumtext ntakiona cha mtema kuni
kumbe umelisi kwa dingi ako ujogoo eeh..