MADIBA MANDELA
JF-Expert Member
- Mar 2, 2014
- 503
- 398
Jana nilieleza machache kuhusu korosho. Leo ngoja niongeze 'nondo' kidogo;
Kwanza nipongeze serikali kwa kuamua kuwanusuru wakulima kwa kununua korosho yao, ili kuwaepusha na hasara ikiwa wafanyabiashara 'watagoma' kununua. Lakini mpango huu wa serikali sio sustainable. Ni zimamoto ambayo haiwezi kutumika siku za mbeleni. Letz asume mwakani bei ya korosho ikazidi kuporomoka kwenye soko la dunia, je serikali itazinunua tena? Ikumbukwe wanunuzi wakubwa wa korosho duniani bado wana stock kubwa ya mwaka jana na hivyo mwaka huu wamenunua kiasi kidogo sana.
Demand ya korosho sio kubwa kwenye soko la dunia ndiyo maana bei imeporomoka (the higher the supply and the lower the demand, the price tends to fall). Hii ni principle ya uchumi wala tatizo sio wanunuzi wa korosho kugoma kununua. Nao wanaangalia faida. Wasije kununua wakapata hasara maana huko duniani bei inazidi kuporomoka kila siku.
Ivory cost mzalishaji wa tatu wa korosho duniani mwaka huu alizalisha tani 770,000 lakini kauza tani 400,000 tu. Anazo tani zaidi ya 370,000 ambazo hajui pa kuzipeleka. Ameamua kuanzisha viwanda vya kufanya processing ili kuiongezea thamani korosho yake. Ni vizuri Rais wetu ashauriwe katika hili badala ya kuwalaumu tu wafanyabiashara.
Pili, serikali inahitaji shilingi Bilioni 600 kuweza kununua tani laki mbili za korosho zilizopo Mtwara. Fedha hizi zinapaswa kuidhinishwa na bunge. Ubabe ukitumika zikatoka bila bunge kushirikishwa itakuwa ni kukiuka misingi ya utawala bora. Impact yake ni kubwa.!
Tatu; Hizi Bilioni 600 zitatoka hazina. Kama serikali isingevunja mfuko wa maendeleo ya korosho maana yake hizi fedha zingetoka kwenye mfuko huo (through export levy). Halafu hizi za Hazina zingefanya mambo mambo mengine kama kuboresha miundombinu, kuongezea watumishi mishahara etc. Maana yake ni kwamba mfuko wa maendeleo ya korosho ndio ulikua 'sustaibable solution' ya hii crisis. Hata bei ingezidi kuporomoka kwenye soko la dunia kwa miaka ijayo, mfuko huu ulikua na uwezo wa kuwafidia wakulima kwa kufanya 'topup' kwenye bei itakayotangazwa na wafanyabiashara.
Lakini hii ya kukomba fedha hazina kwenda kununua korosho sio mbinu 'sustainable' kwa sababu hatuwezi kila mwaka kusimamisha shughuli za maendeleo ili kwenda kununua korosho. Ndio maana nasema hii ni zimamoto na itafanya kazi mwaka huu tu. Mwakani bei ikiporomoka tena serikali haitakuwa na uwezo wa kutoa Bilioni 600 zingine kununua korosho.
Nne; Serikali inasomba korosho kuzipeleka wapi? Dar hakuna soko. Huko duniani bei imeporomoka. Sasa serikali inazisomba kuja Dar ili iweje? Kama lengo ni kuzinunua na kuziweka kwenye maghala hadi bei itakapokuwa nzuri, kwanini isitafute maghala hukohuko Mtwara ili kupunguza gharama? Kwanini zije Dar? Zinakuja kufanya nini?
Tano; Rais amekagua magari 75 ya jeshi kwa ajili ya kubebea korosho. Kila gari lina uwezo wa kubeba tani 20. Maana yake ni kwamba kila trip moja magari hayo yatasomba tani 1500. So ili kumaliza korosho yote magari hayo yatakwenda trip 133. Kila trip moja itahitaji kama siku 3 hivi (siku moja kwenda Mtwara, siku moja ya kupakia na moja kurudi Dar). Thatz under ceteris peribus. Hatujaweka siku za service, kuchelewa kupakia/kupakua, gari kuharibika, mvua etc.
Ukichukua siku 3 kwa kila trip ukazidisha kwa trip 133 utapata siku 400 ambazo ni kama mwaka mmoja na mwezi mmoja. Yani tutatumia mwaka mmoja na zaidi kubeba tani laki mbili za korosho kutoka Mtwara kuja Dar. Zikishafika Dar hata bei ikipanda kwenye soko la dunia hatutaweza kuziuza kwa faida maana tutakuwa tumetumia gharama nyingi sana kuzisafirisha (fedha, muda, nguvukazi, mafuta ya magari etc). Sidhani kama Rais ameshauriwa vizuri katika hili. Kuna haja ya kutafakari upya.!