Niite popote katika jiji la DSM, nitakutengenezea bure kabisa computer yako

faru joni

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
478
Reaction score
734
Habarini ndugu zangu wana jamiiforum, poleni na miangaiko ya kila siku kuakikisha tunajenga Tanzania mpya.

Nielekee kwenye dhumuni la mada:

Kulingana na changamoto za kukosa ajira, kukosa mtaji na kutokuwa na chochote kile katika maisha yangu,

Nimefikilia kutoa msaada wa kutengeneza bure kabisa computer upande wa SOFTWARE TU, na nitakupa ushauri juu ya tatizo la HARDWARE kama lipo, popote pale katika jiji ili la Dar es salaam

Malipo yako utakayonilipa ni nauli ya kufika ulipo na kurudi nilipotoka na chakula tu (hapa naamanisha chochote utakachokuwa nacho).

Nakaa: MBEZI MSAKUZI (MOROGORO ROAD)-DSM

Elimu: DEGREE

Phone number: 0755836347

Natanguliza shukrani zaangu kwenu nyote, mungu awabariki sana

Karibuni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante mkuu kwa taarifa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umejiongeza mkuu tatizo linaweza kuwa la 20k kutengeneza ,ukiitwa nauli na posho plus Asante inaweza kufika 60k.

Mjini mipango

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umejiongeza mkuu tatizo linaweza kuwa la 20k kutengeneza ,ukiitwa nauli na posho plus Asante inaweza kufika 60k.

Mjini mipango

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu computer yako ntakutengenezea bure kabisa, sidhani kama hapa jijini dar es salaam kuna sehemu nauli inaweza kufika ata elfu 10 kwa daladala

Kuhusu ela ya chakula ni chochote utakachokuwa nacho ata ukiamua kunipa elfu 2000 nitashukuru mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsante mkuu mi nitakutafuta computer la nyumbani linasumbua sana niki log off na kuzima umeme, niliwasha lina -behave as if nimelizima kwa short cut
tatizo la pili ile software ya sauti inabiti iwe installed
Tatizo la tatu nikitumia modem ya internet inagoma. nitakuelekeza home uje unirekebshie kama utaweza hizo changamoto
 
Mbezi-Mbagala/Tegeta gharama za foleni unaziweka wapi!?.. Mbona kama unatwanga maji kwenye kinu mzee!.
 
Sawa mkuu, nitayamudu wala usjali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbezi-Mbagala/Tegeta gharama za foleni unaziweka wapi!?.. Mbona kama unatwanga maji kwenye kinu mzee!.
Mkuu waswahili wanasema mtembea bure sio sawa na mkaa bure, now sina kazi kabisa nimeshazunguka kwenye maofisi mbalimbali ata kazi za viwandani nimekosa

Nikitoka mbezi asubuhi au muda wowote kukufata wewe uliopo mfano mbagala nikatumia masaa 2 kuja uko nikakutengenezea kifaha chako ukanipa ela ya chakula tu

Na kuendelea kukaa tu mtaani sina chochote, sina pa kwenda sina wa kumlilia hali kipi bora?

Sina mtaji kabisa wa kusema nafanya au nianze biashara

Ebu nishauri ndugu yangu nifanyeje, maana unaweza nishauri kitu bora zaidi ya ninachofikilia ndugu yangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbezi-Mbagala/Tegeta gharama za foleni unaziweka wapi!?.. Mbona kama unatwanga maji kwenye kinu mzee!.
Hizo zote ni strategy plan za muuza karanga kuwaonjesha wateja then ataanza kuwacharge ASAP
 
Umepanga au unakaa kwenu!?.. Me kwa ushauri wangu kama una utaalam wa hiyo fani kweli, nenda kariakoo kaunge urafiki na mafundi wa pale, mostly hawana utaalam wa PCs lakini wanategemeana so iwapo upo vizuri kichwani basi utageuka tegemeo lao na mwisho wa siku hutakosa hela ya siku!.
Kwenye red nimesense umepanga kutafuta sympathy za wateja wako as watakuonea aibu wakupe cha juu!, kama ni hivyo basi tambua wateja mostly ni viumbe katili kwenye biashara!..

Kariakoo ni njia yako kutoboa ukiwa serious!..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…