“Niiteni Raila Amolo Odinga”

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Amesema anaona watu wakipata taabu sana kuhusu namna watakavyomuita kwa kuwa hayuko serikalini kwa sasa. Anasema yeye ana jina yale halisi, watumie hilo.
Nairobi. Kiongozi wa Muungano wa Mageuzi na Demokrasia (Cord), RailaOdinga, amewataka watu wasisumbuke bure jinsi watakavyomwita, kwa kuwa hahitaji ‘huruma za watu’.
Alisema kuwa ameyaweka nyuma yaliyoibuka kutokana na mvutano wa Uchaguzi Mkuu wa mwezi uliopita na kuwakosoa wale wenye utata kuhusu jinsi watakavyomwita mbele ya umma.
“Nimeketi hapa na kutazama jinsi kila mtu akitatizika atakavyoniita. Yeyote asisumbuke kusema mimi ni nani wa zamani. Mimi ni Raila Amolo Odinga,” alisema.
Odinga alikuwa akizungumza katika shule ya msingi ya Onjiko eneo Bunge la Nyando, Kaunti ya Kisumu, wakati wa mazishi ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama cha Walimu nchini Kenya, (Knut) David Okuta.
Watu waliosimama kuzungumza kabla yake walitatizika kumtaja. Baadhi walimwita Waziri Mkuu mstaafu huku wengine wakimwitia ‘Aliyekuwa Waziri Mkuu’ na hata wapo waliomwita moja kwa moja ‘Waziri Mkuu’.
Wadhifa wa Waziri Mkuu uliondolewa na Katiba, ambayo iliuvumilia hadi Serikali ya mseto ilipovunjika rasmi Machi 9, Rais Uhuru Kenyatta alipoapishwa.
Hata Rais Kenyatta aliposimama kuhutubia alimtaja Odinga kuwa ‘Ndugu yangu Waziri Mkuu’.
Alipozungumza kabla ya kumkaribisha Rais, Odinga alilazimika kutumia lugha yake ya asili kuwahakikishia wafuasi wake kuwa bado ana umuhimu katika siasa za Kenya.
“Jokanyanam antie pod adhi nyime. Ka oluth kuon otur ok omwon tedo dhi nyime.” (Watu wa ziwa, bado ninaendelea mbele. Kuvunjika kwa mwiko, si mwisho wa kupika ugali). Kisha alirejea msemo huo wa Kiswahili alipowahakikishia wafuasi wake kote nchini kwamba yeye hajaporomoka kisiasa kwa kuwa ataungana na rais mstaafu Mwai Kibaki kwa ajili ya maendeleo.
“Serikali si ya sehemu moja ya Kenya tu ni ya watu wote. Nawasihi Wakenya wote tushirikiane ili kuleta maendeleo katika maeneo yote,” Rais Kenyatta alisema.
Kwa upande wake, Rais Kenyatta alisifu falsafa ya marehemu Osiany katika kupigania maslahi ya walimu.
“Osiany alikuwa akitilia maanani mahitaji ya kitaifa katika kila alilotenda. Nilifurahi kufanya kazi naye,” alisema.
Odinga alimsifu marehemu kwa weledi wake katika kujadili mamboyaliyowahusu walimu na pia kwa msimamo thabiti aliokuwa nao wakati wa kuwatetea aliokuwa anawawakilisha.
Odinga pia alitoa changamoto kwa Serikali iwaajiri walimu 80,000 zaidiili kuziba pengo lililopo kwa sasa.

CHANZO: MWANANCHI
 
Hakuna hakikisho ushirkiano unaitwa wa raila na kenyatta, utadumu. kwanza kaanza kuungana na moi kwa chama cha KANu na baadaye kaleta mapinduzi kimabavu ndani humo, ambayo ilijumuisha wakereketwa mfano marehemu saitoti kutoka na kujenga upinzani.

...mwaka wa 2002, waliamua kuleta ushirikiano kati ya kibaki lakini ushirikiano huo ulivunjika hadi pale kofi annan alileta mkataba wa serikali ya mseto, lakini udhaifu wa ODM unaonekana na hadi wa sasa unajulikana sana hasa katika kushawishi wakenya kuingia madarakani. hii imekuwa kibarua kwao..

si ajabu ODM ambayo sasa ndio CORD imejenga Kioja kingine kwa kutafuta kushirikiana na kenyatta. si ajabu ushirikiano huu ukivunjika hivi karibuni...

Sasa CORD watajaribu kuikwepa electorate na kura za wakenya kwa njia gani???
 

Hakuna uhusiano Uhuru Kenyatta anao uhitaji kutoka kwa Raila Odinga,,isipokua
ule wa kua wote ni wana Kenya.

Uhuru Kenyatta ana uwezo mkubwa katika bunge na kwa hivyo,,,,,,, hamuhitaji
Raila hata kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…