Kaunara
JF-Expert Member
- Feb 4, 2013
- 249
- 452
Kutokana na hali inavyoendelea Duniani ipo siku hayawi hayawi yatakua.
Nimeangalia movie nyingi za world war II pia mauji ya Rwanda. Ukweli familia nyingi hazikujiandaa walidhani ni uzushi haliwezi kutokea. Wale ambao waliamini lingeweza kutokea wengi watusi walikimbia nchi yao na kwenda nchi za jirani. Hata waisrael nao wengi walikimbia na kwenda nchi za jirani. Kuna wale ambao walijificha kwenye majumba yao kipindi chote hicho.
Baada ya vita ya pili kuisha wazungu wamejiwekea utaratibu wa kujenga sehemu ya kujificha wakati wa shida katika nyumba zao. Namaanisha underground bunker ndani ya nyumba.
Shida ipo kwetu Waafrika. Tumekuwa tukijenga majumba mazuri sana ila hamna sehemu ya kujificha na familia zetu tukiamini dunia ni sehemu salama kabisa na Tanzania ni nchi ya amani.
likitokea la kutokea umejiandaa vipi na familia yako? Ni wapi unaweza jificha hata mwezi mmoja kujiokoa wewe na familia yako?