Ukweli mtupu, Hii mada ni pana, kuna haja ya kuandikia thread/makala yake ya kujitegemea. Ahsante kwa mchango wako.Juice za viwandani ndio mauaji ya halaiki yaani baada ya miaka michache hili taifa sijui litabaki na kina nani????
Unakuta eti mtu hanywi pombe jambo jema kabisa halafu anakunywa kopo zima la Azam juice peke yake kwenye masherehe na mwingine anapewa makopo 2 na anajisifu eti alichangia fedha kubwa halafu asinywe wee.. Yaani mchango wako mwenyewe unakuuaa?
Ana unafuu mlevi kuliko mnywa juice 🧃 ilijazwa masukari ya viwandani na masweetener hatari kabisa.
Vifo vya kujiua Tanzania ni vingi mno mno sijui huko kwa Mungu Tutajibu nini??
Nimepata solution, anza kunywa Sparkling water. Yaani very simple.
Hapo tupo pamoja iwapo itakua chai bila sukari.!Hoja: Unaacha soda unakunywa chai na kahawa.! Are you serious.?
Jibu : Hatumaanishi Chai (majani ya Chai) iliyowekwa Sukari, Mfano mimi binafsi natumia kahawa iliyowekwa Tangawizi bila sukari.
=
Soda ni kalori nyingi na ina sukari nyingi, ambayo inaweza kusababisha uzito kupita kiasi na unene wa kupindukia. Pia inaweza kuongeza hatari ya magonjwa ya moyo, kiharusi, na aina fulani za saratani.
Ikiwa unatafuta njia mbadala ya soda, chai na kahawa ni chaguo nzuri. Unaweza kutengeneza chai au kahawa bila sukari kwa kutumia asali, stevia, au matunda.
Kwa mfano, unaweza kutengeneza chai nyeusi na asali, chai ya kijani na tangawizi, au kahawa na maziwa ya soya. Unaweza pia kuongeza viungo kama vile tangawizi, karafuu, au mdalasini kwenye chai au kahawa yako ili kuongeza ladha.
Mimi nilikuwa nakunywa soda 3/4 kwa siku...Wakuu, wakubwa kwa wadogo naomba kujua madhara nitakayopata kwa unywaji wa soda, nimekua kama teja, kuna wakati nanunua majiyakuywa na soda pembeni yan kwanza nakuywa soda nikiridhika ndo nakuywa maji kidogo.
Nilianza kwa kuywa soda chupa moja wakati wa mchana tuu saivi naweza kuywa mara3 kwa siku, nimefikia hatua nanunua cret la soda kwajili ya usiku kabla ya kulala niwe napiga moja then naenda on bed, nina khofu nikitu gani kitafata baadae ila kwa sasa sina tatizo lolote.
Ugojwa wangu ni Mirinda nyeusi, Sprite, Stone tangawizi au pineapple pia energy drinks hua nagonga maramoja moja kama nikiywa soda then nikawa sijaridhika.
Mimi nilikuwa nakunywa soda 3/4 kwa siku...
Ile kitu inaitwa Pepsi....Uweeeeeh!!!!
Ila sasa hivi soda nzima simalizi...soda moja nakunywa siku mbili...naweza kumaliza wiki sijanywa soda kabisa.
Kitu gani kilinisaidia....Nilianza kupenda chai/kahawa...nikipata hamu ya soda tu nakoroga kahawa au chai nakunywa....kidogo kidogo kupenda soda nikaanza kupunguza hadi sasa..
Na wewe unaweza kufanya hivyo pia...Itakusaidia..kama unapenda kunywa maji kwa wingi unaweza kutumia kama mbadala wa chai..
Kila lenye kheri Mkuu...