Kuna mwanamke amebeba mimba mara mbili na anazaa kabla ya wakati na watoto anao wazaa huwa awachukui hata wiki wanakufa HIVI SABABU GANI ZINAZO FANYA TATIZO KAMA HILO KUTOKEA.
Kujifungua kabla ya wakati, Tatizo hutokana na sababu mbalinbali mojawapo inawezekana kuwa sababu zinazotokana na mama mwenyewe mfano; Kifafa cha mimba, umri kuwa mdogo, magonjwa mbalimbali wakati wa ujauzito mfano mfumo wa jinga ya mwili, mfumo wa damu, vivimbe/uvimbe wakati wa ujauzito, pia inaweza kuwa uwepo wa mapacha,..kutegemeana na maelezo ya mgonjwa/mjamzito na vipimo inawezekana kubainisha tayizo ni nini hasa.
Uwezekano wa kujitokeza kwa tatizo hili kama kuna mtu wa karibu wa familia(ndugu/ukoo), au kujirudia iwapo ilitokea katika mimba zilizopita.
Kufa kwa watoto waliozaliwa kabla ya muda wao, hutokana na matatizo mengi lakini kubwa hasa ni magonjwa shambulizi na upungufu/kushindwa kuhifadhi joto kwa watoto hawa.
Kuna mwanamke amebeba mimba mara mbili na anazaa kabla ya wakati na watoto anao wazaa huwa awachukui hata wiki wanakufa HIVI SABABU GANI ZINAZO FANYA TATIZO KAMA HILO KUTOKEA.
Sababu ni nyingi.....ila mojawapo inaweza kuwa ni rhesus factor.....kama mama ana negative rh factor basi inakuwa tatizo kwenye ujauzito....ila kuna asilimia ndogo sana kwa waafrika ambayo ni kama 10%....wengi wanakuwa whites...ambapo hata akijifungua mtoto anakufa mapema sana.