Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,421
Nilikuwa nimetoka shule ya sekondari ya Pugu, ambako nilienda kumwona ndugu yangu anayesoma pale. Nakumbuka ilikuwa ni Jumapili mwaka 1999. Nilipanda basi kurudi mjini baada ya mazungumzo na huyo ndugu yangu. Wakati nikiwa kwenye basi, alipanda abiria mmoja ambaye alionekana kuutwika mtindi. Kwa Jumapili jioni, huwezi kushangaa kukuta mtu kautwika mtungi saa 11 jioni. Yule bwana kwa bahati mbaya akaja kukaa kwenye kiti nilichokuwa nimekaa.
Alipokaa hakunisalimia, bali alinitazama sana, yaani kwa muda mrefu hadi nikakereka. Halafu alisema, ‘usinitishe bwana, kwani nimefanya nini. Kama mambo yalishaisha sasa kwani ni lazima uyaendeleze.' Nilishangaa, kwa sababu nilikuwa simfahamu na sikuwa naelewa anachosema. Aliendelea, ‘sikiliza afande, najua leo umenishika, lakini mambo si yalishaisha, hela zake nilimrudishia, basi kama unaona kunikamata ndio utafaidi, sawa nikamate niko tayari.' Sikumwelewa, lakini nilihisi kwamba ananichanganya na polisi fulani.
Niliona nimchanganye tu na yeye. ‘Kwa nini ulizichukuwa hela zile?' Nilimuuliza. ‘Wewe mwenyewe unajua usawa wa nyumbani, ungekuwa hutujui sawa. Wewe mwenyewe unamchukua mamangu mdogo anakupa stori za homu, sasa unauliza kwa nini nilizichukuwa, si shida.' Niliona naanza kuadhirika kwa sababu abiria wengi waligeuka kumtazama huyo afande anayemchukuwa mama mdogo wa yule mlevi ambaye pia alishajitangazia kuwa ni kibaka. ‘Sawa, nimeelewa, yameisha, sina haja ya kukukamata.' Nilisema nikijua yameisha, kumbe yalikuwa ndiyo yanaanza.
Aliniambia, ‘lakini afande wewe siyo mchezo. Mama yangu unamchukuwa, sista umebamba, haikutosha, mama Mona naye hukuachia, halafu yule demu mwenye grosari karibu na mtendeni shop ukabeba. Haki ya Mungu afande unaniacha hoi, unafagia...! lakini angalia ukimwi, angalia afande....!'
‘Kama usiponyamaza nitakukamata nikurundike ndani,' nilisema nikiwa nimekereka. Niligundua kwamba, mtu anaweza kufanya jambo kimzaha, likageuka hadi mwenyewe akalihisi kama ni kweli. Nilijuta kumjibu kwa kujifanya mimi ni huyo afande kweli.
‘Hapo sasa ndiyo sikuelewi. Wewe siri zako zikianikwa unatishia kuniaresti. Mimi nimesema ukweli tu, lakini unakuwa mkali, wala sijakosea wala nini, na wala sitamtonya mama mdogo kwamba wewe ni kifyagio. Kwanza nilipie nauli.' Alisema.
Nilitoa nauli haraka na kumlipia. ‘hapo sasa sawa. Simwambii mama mdogo wala sista, wewe swaga tu, wanawake wa mjini nao wanapenda mkwanja sana...' Alisema na kusimama. Alikuwa amefika. Alishuka huku akisema, ‘lakini afande angalia, ngoma, kilo mbili hatari...' Abiria wote sasa macho yalikuwa kwangu. ‘Uzuri wa ulevi ndio huo,.. unampa mtu ukweli wake bila kujali,'abiria mmoja alisema. Sikutaka kujibu, sikutaka yawe makubwa zaidi.
Hii kusema cha ukweli inanihusu mimi mwenyewe na wala sio rafiki yangu…………..LOL