Nikaribisheni JamiiForums

Vitamin K

Senior Member
Joined
Dec 2, 2017
Posts
158
Reaction score
168
Habari za muda huu wote wapenzi wa mtandao huu

Nimejiunga na huu mtandao mnamo Dec 2, 2017. Nimefurahishwa sana na namna mijadala inavyoendeshwa humu na nimehasika sana.
Tangu nijiunge nilikuwa nashindwa namna ya kuanzisha mada kwani na mimi baada ya kuona mada mbalimbali zinaletwa humu na kujadiliwa nikavutiwa sana.
Nikasema ngoja nivute subira kidogo nione na kuchunguza namna ya kuanzisha mada na hatimaye nikajua. Pia nikagundua kuna sehemu maalum kwa kila mada inayoletwa humu
Bahati nzuri kwenye kuangalia hizo sehemu nikakutana na hii sehemu ambayo ni ya utambulisho, basi nikasema ngoja nianzie hapa kujaribu kuleta mada japo kwa kujifunza.
Ni matumaini yangu mtanipa ushirikiano kuyajua mambo mengine yanayohusu mtandao huu kwani kila sehemu lazima pawepo na utaratibu wake

Ahsanteni sana!
 
Welcome!
Ila humu huwa hatutumii MATUSI, WALA LUGHA MBOVU NA KEJELI.
 
Hizi karbu za kuomba hizi!! mmmmmhh zinanipa mashaka[emoji23] - karibu japo jina lako mweeee k!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…